RAIS WA TANZANIA AJAYE (TULIYE NA HAMU KUBWA KUMPATA CHINI YA KATIBA MPYA) ATAPATIKANA TU KWA MISINGI YA USHINDANI MKALI NA UBORA WA SIFA ZA MGOMBEA NA WALA SI KUPANGA LOLOTE KABLA YA SIKU YA MNADA!!!
Sawa tu, kwani shida iko wapi??? Ni sifa tu ndizo zitakazogomba laa sivyo hakuzuiliwi mtu hapa.
Isipokua ikumbukwe kwamba tulihiari wenyewe kuingia na kushiriki mfumo mpya wa vyama vingi ambapo kikubwa zaidi ni kwamba kila kitu ni sharti kiendeshwe KIUSHINDANI na wala si kutengeana viti kama ambavyo tulivyozoea huko nyuma kwenye mfumo wa chama kimoja ambapo competitive edge ilikua ni kwa misingi ya POLITICAL MONOPOLY of decisions and destinies.
Kwa mantiki hii, mpangilio wa ndani ya chama fulani kujiamulia kwamba wao wanajipangia rais atoke mkoa fulani au kona fulani ya nchi kamwe haitoathiri NDHANA MPYA WA SIASA ZA USHINDANI ambapo sheria kuu ya mchezo katika Mfumo huu mpya ni kule Wapiga Kura, Vyama Vya siasa na Wagombea wenyewe wa nafasi mbali mbali nchini KUTOKUACHA MWANYA WOWOTE WA KUHISIWA kukaa mahala na kupanga bei (wagombea gani washiriki) na hivyo kufanya kushindwa kwa Soko la Siasa KUTOKUA HURIA na hata nguvu za Demand and Supply kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Wenye wagombea wenu wa urais kichwani, CCM na vyama vya upinzani, kumbukeni kwamba siku zote Ng'ombe Hanenepeshwi siku ya Mnada hivyo fanyeni kazi na kujaribu kuonyesha YOUR BEST tangu hivi sasa maana huko mbeleni hakutokwepo na SHORT-CUTS (Uchakachuaji) tena wala kutafutwa kwa SECOND CHANCE kama hivi sasa Mhe Kikwete anavyolihangaikia na kulilalamikia usiku na mchana kwa CHADEMA.
Lamsingi, tunaposema Tanzania ! nimetowa hoja juu ya hali iliotanguliya toka kuanza vyama vingi!
Ikiwa tutakuwa na Tanganyika, hakuna ugomvi, lakini kitu Tanzania ni Muungano na kila mwenye hisa katika muungano ana haki sawa na mwenziye. Ni kwa mantiki hii ndio zanzibar ina haki ya kuwa na mgombeya wa Tanzania. Ama hoja ya wazanzibari wana Raisi wao, ni sehemu ya mapungufu! kwani hana madaraka Bara, na kinyume chake, wabara ana madaraka visiwani!
Mkuu.Vipi yakhe? Mnataka mle kwenu na kwetu pia? Mnaye rais wa Zanzibar na makamu wake. Mnae makamu rais wa mwungano ambaye ni Mzanzibari. Mbona mnakuwa waroho?
Mkuu.
Ninyi endeleeni na kujadili katiba mpya na Muungano na muundo wake.
mukishindwa kutumia bahati hii iliyojitokeza ndio musahau kuona rais wa serikali ya TZ kutoka Zanzibar.
Kama nchi moja mbia wa muungano, ninyi munaweza kuja na proposal ya ku-rotate huo urais wa Muungano.
Kama munao wanasheria wazuri basi watumieni ili kuweka hoja hiyo kisheria lakini musije mukachukua mawakali kama wa Tanesco kwenye kesi ya dowans! Itakula kwenu.
SpeakerZanzibar ya nini?
Wana raisi wao mimi naitaka Tanganyika yangu,...sioni umuhimu wa Zanzibar zaidi ni mzigo kwetu, wana feed on us kama kupe kwenye ng'ombe!
Afu leo waongoze Tanganyika? Kwanza nani huyo wa kuongoza Tanganyika toka zanzibar?
Gi'me a break
Mkuu.
Mimi nafikiri hoja aliyoleta mleta mada inahitaji tafakari.
kwa sababu gani?
Wanazungumzia Serikali ya Muungano.
Kweli wao wanae Rais wao, rais wa Zanzibar.
Sisi tunapokimbia kujifanyia self criticism basi tutabaki katika kuwakejeli Wazanzibari au kujenga chuki ambayo inatokana na uvivu wetu wa kufikiri.
Vipi wao wawe na serikali ya Zanzibar ,sisi tusiwe na serikali yetu ya "Tanganyika" aka Tanzania bara?
Kama tunachukua jukumu hili la kufikiri basi itatupelekea kuwataka wabunge wetu wa "Tanzania bara" waturejeshee serikali yetu ya Tanganyika.
Hii serikali ya Muungano inaweza kuchukua models za EAC au EU na hivyo kutuondoshea huu unafiki na usanii tulionao leo.
Lazima ifike siku na muda tuseme ukweli, tusiendelee kujidanganya.
Why our union should be so special and unique yet so complicated and itching?
Mtwike.Nadhani tatizo ni jina la hiki kacheo cha raisi wa Zanzibar! hivi ana madaraka gani zaidi ya Mkuu wa Mkoa? ni kiini macho tu, eti ana bendera ana wimbo wa taifa, anapiga baruti 21 akipokeya mgeni, lakini ana Nchi ikiwa haina "sovoreignity"?
Mtwike.
Tatizo ni tatizo lakini kujua tatizo ndio mwanzo wa kupata mwanga wa kutatua tatizo lenyewe.
kwangu mimi hilo si tatizo kubwa. Ni tatizo la kujitakia.
Hapo Zamani za kale...miaka 47 iliyopita nchi mbili ziliunganisha mambo kumi na moja. muungano wa mambo hayo ukazaa Muungano ulioitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Baadaya ya miezi kupita , yule mjanja mmoja akasema ,Hili jina ni refu kwa hiyo tuyaunganishe...Akatutengenezea jina Tanzania...kwa bahati mbaya jina moja la nchi mbia likasukumwa chini ya zulia. na kila anayelitaja anaonekana ni mhaini.
Kale kanchi kengine kadogo kikaendelea kutumia jina lake.
Sasa kama kanchi kadogo hakistahili tena kuwa nchi sasa kiwe kamkoa hili kweli ni tatizo, tena sio tatizo dogo....yaani hata kama ningekuwa mimi ndio mmoja wa wananchi wa nchi hiyo..ningepigana na yeyote ambaye anataka kanchi kangu kawe mkoa.
Guys, we have a big problem here.
Vipi ungeweza kunishawishi, nchi inayofanya muungano na nchi nyengine ikubali kuwa mkoa?
Halafu usiri wa kutoonekana hati original ya makubaliano ya Muungano pia yanaongeza kiwingu juu ya tatizo hili la kujitakia.
At the time Zanzibar was insecure. If the sultan had organised himself and sought assistance from his kith and kin in the Middle East he could have retaken the islands back. Karume new that and that is why he agreed to the Union. He was not forced. He wanted protection. Now that they are sure the sultan is not coming back they can't stop whining. I sincerely believe even today Zanzibar is getting more out of the Union than Tanganyika. What would we lose if the union broke down? I would say 'not much'. What would they lose if the union broke down? Quite a lot ..... residences on mainland (every Zenj leader has at least one house on mainland), businesses (wapemba shops), land (they are entitled to land on mainland but we are not in Zanzibar), cheap goods (especially foodstuffs. Most of their food is sourced from mainland tax free), political positions and influence (they have MPs in the Union Parliament which also happens to be the Tanganyika Parliament. They therefore make laws for us. We don't have representation in their Baraza la Wawakilishi. Lets face it. Being in the Union gives them clout on the international stage which they otherwise would have as an island nation). I think we should grant them their wish to break the union and then tighten the screws on other fronts to let them learn the real facts instead of political demagoguery.Hili si tatizo la kujitakia bro, ni tatizo lilopangwa!
Mwezi mmoja tu baada ya Muingereza kutoa Uhuru, nchi yapinduliwa na waliowengi, miezi Mitatu kanchi kaungana na nchi kubwa zaidi ya mara Mia kiiukubwa na idadi ya Raiya, upanda wa pili wa bahari tena hawana common tribe wala common culture! yote haya kujitakia? call a spade a ........
At the time Zanzibar was insecure. If the sultan had organised himself and sought assistance from his kith and kin in the Middle East he could have retaken the islands back. Karume new that and that is why he agreed to the Union. He was not forced. He wanted protection. Now that they are sure the sultan is not coming back they can't stop whining. I sincerely believe even today Zanzibar is getting more out of the Union than Tanganyika. What would we lose if the union broke down? I would say 'not much'. What would they lose if the union broke down? Quite a lot ..... residences on mainland (every Zenj leader has at least one house on mainland), businesses (wapemba shops), land (they are entitled to land on mainland but we are not in Zanzibar), cheap goods (especially foodstuffs. Most of their food is sourced from mainland tax free), political positions and influence (they have MPs in the Union Parliament which also happens to be the Tanganyika Parliament. They therefore make laws for us. We don't have representation in their Baraza la Wawakilishi. Lets face it. Being in the Union gives them clout on the international stage which they otherwise would have as an island nation). I think we should grant them their wish to break the union and then tighten the screws on other fronts to let them learn the real facts instead of political demagoguery.
ULAGHAI WA KIKWETE KUHUSU KUUNDWA KWA KATIBA YENYE WANANCHI KWENYE STERINGI SASA TUNASEMA BASI: TUNATAKA SERIKALI YA MPITO KUSHUGHULIKIA KATIBA NCHINI NA KUKAMILISHA KILA KITU 2014
CHADEMA,Asasi za Kiraia nchini, Vyuo Vikuu na Nchi Wahisani tunaomba mtuelewe kwamba sasa uzalendo umetushinda na huu utani wote na kiburi ya Mhe Kikwete - tunataka serikali mpya ya mpito sasa hivi kushughulikia katiba!!!
Wananchi; kila mmoja mahala ulipo wakati umefika wa kuachana na mchezo katika mambo ya msingi ambayo tumejaribu kutafuta kiungwana ndio hivo imeshindikana. Hakuna haja kuendelea kubisha mlango usiofunguliwa bali hapa ni kutafuta njia njingine kabisa kwa uwezo wa Nguvu ya Umma.
Cha msingi sasa sisi wenyewe tena vijana, kwa njia zetu zile, TUNAIPA SERIKALI YA Mhe Kikwete hadi April 08, 2011 iwe imewashirikisha wadau wote na mawazo yetu, katika hatua zote za ushiriki, usimamizi na uendeshaji wa mambo ya katiba kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na wala si kutulazimiza na matakwa ya watawala ambao ndio haswa tunaowalalamikia kwa unyanyasaji.
Vijana tuliowengi nchini tusimame kutetea haki zetu kwani haki hapewi mtu hata siku moja. Endpo serikali haitotii hayo maoni yetu basi Vijana kote nchini pamoja na taasisi marafiki wa UTAWALA WA KIDEMOKRASIA NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI MOJA KWA MOJA tujiweke tayari kwa maandamano ya amani kote nchini mpaka matakwa haya yatimizwe au serikali inaposhindwa basi ikatupishe njia haraka!!
Tunasema katika huu mzaha wa serikali kuhusu tume HURU YA BUNGE kugeuzwa kuwa TUME TEGEMEZI YA RAIS ikibarikiwa na Bunge; Vijana tumefika Tamati tena hadi hapa!!!
Kumbe Kupatikana kwa Katiba Mpya chini ya Uongozi wa CCM haiwezikani bila serikali kututwisha MADALALI kwenye mambo ya kuundwa kwa Katiba Mpya nchini.
CHADEMA tusikilizeni, tunahitaji kwana SERIKALI YA MPITO kumbe yenye jukumu moja tu kushughulikia Katiba kwa MUJIBU WA MATAKWA WA WANANCHI katika hatua zote za usimamizi na maamuzi.
BAVICHA na matawi yetu yote ya CHADEMA nchini tueleweni kwamba wananchi sasa tunasema baaasi na Serikali ya CCM iondoke madarakani sasa hivi. Sote tunao uwezo wa kubadilisha haya mambo yote kabla hatujaingizwa porini zaidi.
Mwenye kupata ujumbe huu na akawajulishe vijana wengine 10 juu ya ulaghai uliotangazwa na serikali majuzi kutupora haki ya kusimamia kuundwa kwa katiba mpya bila kuingiliwa na dola.
Lengo lao likiwa ni kuleta katiba waitakayo MAFISADI nchini, kuchelewesha muda tuingie uchaguzi 2015 bila katiba mpya, na vile vile kukiundia CHADEMA mikesi ya kuchonga kisiasa ili baadhi ya wale tunaowapenda wasigombee.
SASA TUNASEMA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI BARA NA VISIWANI YOTE YAWEZEKANA BILA CCM, TUPISHENI NJIA!!!