2018 FIFA World Cup: Yaliyojiri upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia

Observer

JF HQ
Joined
Oct 18, 2006
Posts
189
Reaction score
299
Wanabodi,

Leo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Africa Mashariki kutakua na tukio la upangaji wa makundi ya timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Russia.

Katika michuano hiyo timu 32 zitashiriki kutoka mabara tofauti, huku Africa tukiwakilishwa na nchi tano ambazo ni; Egypt, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia.

Je ungependa timu za Africa zipangiwe na timu zipi? na je nafasi ya timu zetu za Africa kufanya vizuri ni ipi?

Nchi gani unanipa nafasi kubwa ya kuchukua kombe hilo?

Timu zilizofanikiwa kungia kwenye michuano hiyo ni:

Kutoka bara la Africa: Egypt, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia

Kutoka bara la Asia: Austraria, Iran, Japan, Korea Republic na Saudi Arabia

Kutoka bara la Ulaya: Belgium, Croatia, Denmark, England, France, Germany, Iceland, Poland, Portugal, Russia, Serbia, Spain, Sweden, Switzerland

Kutoka bara North,Central America na Carribean: Costa Rica, Mexico na Panama

Kutoka bara la America Kusini: Argentina, Brazil, Colombia, Peru na Uruguay

Tujumuike kwa pamoja wakati tukifuatilia upangaji huo wa makundi

Updates

Group A: Russia, Uruguay, Egypt, Saudi Arabia

Group B: Portugal, Spain, Iran, Morocco

Group C: France, Peru, Denmark, Australia

Group D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria

Group E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia

Group F: Germany, Mexico, Sweden, Korea Republic

Group G: Belgium, England, Tunisia, Panama

Group F: Poland, Colombia, Senegal, Japan

 
Africa tunawakilishwa na waarab wengi. [emoji51][emoji51]
 
Sijajua kwa nini spain mabingwa wa 2010 wawekwe pot no 2. Poland aakae pot no 1. Kama ni kumaliza mshindi wa kwanza kwenye kundi spain alimaliza wa kwanza juu ya Italia.

Kama ni fifa ranking sidhani kama poland atakuwa juu ya Spain. Kigezo gani kimetumika?
 
Wanaotumia azamtv kuna channel itakayoonyesha???
 
Pot zimepangwa kwa mujibu wa 2017 October Fifa Ranking.
 
Afrika mashariki naomba watuweke kundi C pls
 
Mimi sitaki timu za Africa zipangwe na timu kutoka Amerika ya Kusini labda round ya pili
 
Muda ndio huo unataradadi. Dk 30 tu kutoka sasa tunaenda kuona live nani kumvaa nani.

God bless Argentina
 
Wamechanganya timu bora nazile za kawaida ili kwenye droo isije tokea timu bora au vibonde wakaangukia sehemu moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…