Natangaza vita na huyu adui popote pale nitakapomuona. Na nimejipanga kwelikweli! Nimejitathmini na kugundua sipendi kuona mtu yoyote akitaabika kwa umasikini. Ukiweza kuushinda umasikini, mambo mengi sana yanakuwa rahisi zaidi kuyakabili na unakuwa mtu bora zaidi.
Hii ndiyo mipango yangu kwa 2018 na jinsi nitakavyomkabili huyu adui (namwambia kabisa mipango yangu, hii inaonyesha jinsi nilivyojipanga!):
- Nitamtanguliza Mungu mbele zaidi
- Nitasaidia wengine walioonyesha nia thabiti na juhudi za kupambana na umasikini (either kwa kuinvest katika biashara zao au kuwapa msaada kama grants/donations katika biashara zao, hata kama ni 10,000/=).
- sitapoteza muda wangu kwa mtu yeyote au jambo lolote lile lisilonisaidia katika mapambano haya. Yeyote atakayenipotezea muda au hela yangu kizembe, nitamwambia wazi na sitamuonea aibu na atalipa kwa kosa hilo kwa njia moja ama nyingine.
- nitajitoa kabisa katika mijadala yote ya kisiasa. Nitarudi kuwa msikilizaji kama ambavyo nimefanya kwa muda mrefu tu. Itakapofika December 2018, naweza hata nisijue Waziri Mkuu ni nani lakini investment zangu zitakapokuwa zinaingiza pesa ya kutosha tu, mbona itapendeza zaidi!
- nitakemea mawazo, kauli au fikra za kimasikini kwa nguvu zangu zote popote pale nitakapozisikia. Hii nitafanya bila woga au kumung'unya maneno. Itafika wakati, umasikini ukiniona tu naingia sehemu ulipo, unakimbia wenyewe! Yes, it's that serious!
- nitafuata kwa nidhamu kubwa dira na muelekeo ninaojiwekea wiki hii ya kwanza ya January 2018. Nitakuwa flexible kiasi katika execution kwa jinsi itakavyobidi lakini nitajitahidi dira na malengo yawe yale yale.
- nitakuwa najikumbusha thamani yangu na kuisimamia kwa nguvu zangu zote kila nitakapokuwa na kila nitakachokuwa nafanya (na kuwafunza wengine pia wajue thamani zao).
- nitatenga muda kuwa nawafundisha wengine na kushare ninachokijua. Hii imekuwa ni passion yangu siku zote ingawa sijaitumia ipasavyo kwa muda sasa.
Nayasema haya wazi ili universe na mbinguni wasikie na inipe msaada wote ninaohitaji katika hili. Natamka pia afya njema ya akili na mwili na amani katika moyo wangu ili nipigane vita hii kwa ujasiri na ushindi wa kishindo.
I DECLARE WAR. UWEZO NINAO, SABABU NINAZO, NIA NINAYO!
Nitarudi December 30, 2018 kuja kutoa testimony itakayotoa watu machozi.
My motto in 2018: 'Everybody around me is rich, or will be'
Happy New Year to you all.