2021 AFCON Special Thread

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Michuano ya Afcon imefika, ni hapo kesho ndio inatarajiwa kuzinduliwa. Itafanyika kuanzia kesho Januari 9 mpaka Februari 6 mwaka huu.

Michuano hii ilibidi ifanyike mwaka jana 2021 ila kwasababu ya Covid-19 ikahairishwa. Hivyo inafanyika mwaka huu ila ina jina la mwaka jana.

Mwenyeji wa michuano hii ni Cameroon, huku Algeria akiwa ni bingwa mtetezi!

Jumla ya timu 24 zitapambana kutafuta bingwa mpya katika michuano itakayifanyika katika majiji matano yenye viwanja sita ndani ya Cameroon.

Mechi hizo zitakuwa live kupitia ving'amuzi vya Azam, Dstv, Star times, Canal.
Wale wadau wa kustream basi pitieni hesgoal.com

Hivyo, kwa updates zote za michuano hiyo utakuwa unazipata kwenye uzi huu karibu sana mwanamichezo!

===========================

Senegal yatwaa ubingwa kwa kuifunga Misri kwa mikwaju 4-2 baada ya kutoka suluhu dakika 120.
 
Ahsante mkuu, wakati naingia hapa nilikuwa nawaza kama ushapandisha uzi. Nisingeuona ningekutag uupandishe.
 
Wapi timu za Afrika Mashariki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…