2023 Achana na kutumia vibubu kuhifadhi fedha, tumia njia hizi

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Mwaka 2023 kama unamalengo ya kufanya jambo lako na lengo lako ni kutumia kibubu kiwe cha bati au cha mbao, njia salama ya kuhifadhi pesa bila usumbufu ni kufungua accounts zifuatazo;

Tigopesa -Kibubu
Airtel Money - Timiza
M pesa - M pawa

Hizi accounts zimenifanyia makubwa sana. Kila siku nilikua nahakikisha naweka hela hata iwe 500, accouts hizi haziingiliani na accounts za fedha kwenye simu.

Watu wanalalamika mara hela yangu kwenye kibubu imechukuliwa na chuma ulete, fungueni hizi accounts mtakuja kunishukuru.
 
Siku ukiibiwa simu ndio utajua kuwa hata huko sio kwema.

Pin ni tarakimu 4 tu mwizi atakuliza mapemaaa.
 
Nidhamu nidhamu nidhamu.

Ukiwa na nidhamu ya pesa hata uwe nayo mkononi huwezi itumia bila malengo.

Mimi sikuweka mkoba ila niliweka mbali mno... Ilikua unaingia menu ya mpesa, unaenda zile huduma za kifedha, unaenda kuweka pesa kwenye account ya benki iliyoingia ubia na vodacom, hapo kuna viprocess kibao mpaka uweke ela tu.

Na kutoa ni process zaidi lakini bado pesa haikukaa mwezi nikatoa.
Usipokua na nidhamu hata ukifukia kaburini utafukua utumie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…