Pre GE2025 2024 haya ndiyo matukio makubwa yanayotegemewa na wanasiasa

Pre GE2025 2024 haya ndiyo matukio makubwa yanayotegemewa na wanasiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Mwaka ndo huu ambao shughuli za wanasiasa kuwa bize zaidi kuliko kipindi kingine

Matukio makubwa ambayo yataambatana na shughuli za wanasiasa ni kama ifuatavyo

1,Vikao majimboni vya usiku na mchana,ng'ombe, kuku mbuzi kuchinjwa ni mwaka huu, tunategemea kuwaona wabunge majimboni mwaka huu wakiwa na vikao hivyo

2,Ni mwaka ambao waganga wa kienyeji wanaenda kuemeka kwa kupiga ramli na kutengeneza njia (chonde chonde msiwaue watu ndugu zetu walemavu)

3,Pesa zitagawiwa, ni kipindi ambacho pesa zitafanya kazi

4,Ni kipindi ambacho tutashuhudia misururu mirefu ofisi na nyumbani kwa mbunge

5, Tutashuhudia harambee za ujenzi hasa maeneo ya dini na harusi

6, Tutashuhudia mbunge anaonekana mara nyingi majimboni kuliko kipindi chochote

7,Tutashuhudia watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha

8, Tutashuhudia walevi wakiongezeka sana hasa nyakati za asubuhi

9, Tutashuhudia watumishi wa umma hasa walimu wakiitwa semina na mbunge na mkurugenzi wa Halmashauri

Ongeza mengine tutakayoshuhudia 2024
 
Back
Top Bottom