JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,229
- 5,285
Hafla ya utoaji wa Tuzo za Shindano la Stories of Change Msimu wa 4 inatarajiwa kufanyika siku Sita kutoka leo yaani Septemba 21, 2024.
Mwaka huu 2024, Washiriki wameonesha uwezo wa juu katika kuijenga 'Tanzania Tuitakayo' wakilenga kuboresha Uchumi, Elimu, Afya, Teknolojia, Kilimo, n.k.
Mbali na Washindi wa Maandiko Bora kupewa zawadi, pia baadhi ya Wazalishaji Bora wa Maudhui ndani ya JamiiForums.com watatambuliwa na kutuzwa kwa mchango wao mkubwa katika Majukwaa yetu ya Kidijitali.