Septemba 21, 2024, tutayatambua Maandiko yaliyoibuka kidedea kwenye Shindano la Uandishi wenye Tija Mtandaoni la Stories of Change ambapo mwaka huu (2024) maandiko yalitoa mapendekezo kuhusu Tanzania Tuitakayo kwa Miaka 5 hadi 25 ijayo kwenye Sekta mbalimbali.
Aidha, katika siku hii Wazalishaji Bora wa Maudhui ndani ya JamiiForums.com watatambuliwa na kupewa tuzo kwa mchango wao Mkubwa jukwaani.