2024 USA Presidential Debate: Joe Biden avaana na Donald Trump kwenye mdahalo wa kwanza kabla ya uchaguzi November 2024

2024 USA Presidential Debate: Joe Biden avaana na Donald Trump kwenye mdahalo wa kwanza kabla ya uchaguzi November 2024

Observer

JF HQ
Joined
Oct 18, 2006
Posts
189
Reaction score
299
Wanabodi,

Leo kutakuwa na mdahalo wa kwanza kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani, November 2024.

Mdahalo huu utawahusisha mgombea wa urais kwa ticket ya Democrat, rais Joe Biden na mpinzani wake Donald Trump kutokea chama cha Republican

Mdahalo huu unatabiliwa kuwa wa moto kutokana na mambo mengi yanayotokea duniani kwa sasa (Vita ya Russia na Ukraine, mgogoro wa Gaza, Misimamo yao kuhusu Taiwan na China)

Mdahalo huo utaanza saa 10 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na utafanyika Atlanta

Mdahao huo umeandaliwa na CNN.

Anacholenga zaidi Trump: Trump anatoa sehemu kubwa ya maoni yake ya umma kwa malalamiko binafsi - akijibu madai yaliyokanushwa kwa muda mrefu ya udanganyifu katika uchaguzi wa 2020, akiwaona waliovamia Ikulu ya Marekani kama wazalendo, na kukemea mashtaka ya uhalifu anayokabiliwa kama ‘kazi za kisiasa’.

Washauri na washirika wa Trump wamemtaka rais huyo wa zamani kuzingatia masuala kama vile uchumi, uhalifu na mfumuko wa bei.

Suala la umri: Biden ni mzee mwenye umri wa miaka 81 na ndiye rais mzee zaidi wa Amerika. Trump ana miaka 78.

IMG_3388.jpeg

IMG_3387.jpeg


Sikiliza kupitia link hii

View: https://www.youtube.com/watch?v=-v-8wJkmwBY
 
Mm bado nimelala fofofo ila nampa kura Mzee Trump, ngoja nikung'ute vumbi passport yangu ya USA nirudi nyumbani kumtoa Biden madarakani.
 
Acha utani mkuu
Niko serious mkuu sio sarcasm ..yangu ime ungua nipo kwenye harakati ya kuchukua ndogo nikute natumia tumia sasa niliona nchi 24 itafaa nka baki njia panda isije kua ndogo sana
 
Trump ni mswahili sana, anaulizwa hiki anajibu kile, anaulizwa kile anajibu mjadala wa nyuma. Nadhani kinacho mbeba sana ni over confidence pamoja na kuwa public speaker mzuri japo battle za nyuma zote alipoteza.

So far natamani kitu kama hiki kingekuja huku kwetu ingekuwa safi sana.
 
Niko serious mkuu sio sarcasm ..yangu ime ungua nipo kwenye harakati ya kuchukua ndogo nikute natumia tumia sasa niliona nchi 24 itafaa nka baki njia panda isije kua ndogo sana
Nch 24 ndogo sana, kama ndogo jitahidi Hadi 32 ,
Ya mdau hapo kama sikosei ni 43
 
Back
Top Bottom