Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Uchumi wa wananchi mmoja mmoja ni mgumu sana, vijana wanashinda vijiweni kwasababu hawana kazi. Wengi hujiingiza katika ulevi , kucheza kamari na kuvuta bange kutokana na kukosa kitu cha kufanya.
Serikali imeweka tozo kila mahali, hawa hawa wasio na kipato maalum bado wanakamuliwa ili kuiongezea serikali pato. Hawa wachumi wetu wanashindwa kufanya tafiti na kuja na jawabu la kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja. Hizi ahadi zipo hata kwenye ilani ya 2020 lakini hazija tekelezwa. Watatuambia nini kipya tuwaamini?
Mpaka sasa hivi sera ya kumtua mama ndoo kichwani bado ni ndoto. Maji salama kupatikana ni changamoto sehemu nyingi za nchi hasa vijijini na hata baadhi ya miji. Kukosekana kwa maji kunazalisha magonjwa wakati uhakika wa matibabu pia haupo.
Wananchi wanaomba huduma za maji, shule, zahanati na barabara, ikitokea mradi mmoja umefanikiwa mfano kujengewa shule, wanyonge watalazimishwa kumshukuru Rais kwa kuwaletea shule kama vile unavyomshukuru Mungu kwa kukupa uhai.
Uchumi wa mtu mmoja mmoja ukiimarika, serikali itajipunguzia mzigo kwani wananchi wakipata viongozi wazuri wanaweza kutatua changamoto zao wenyewe.
Enzi zao la kahawa limeshamiri kule Moshi, wakulima waliacha 10% ya mauzo ya kila gunia katika mfuko wa maendeleo wa kijiji. Baada ya mauzo wanakaa kikao na kijadiliana tatizo lao kubwa linalowakabili kijijini. Kwa njia hii waliweza kujenga shule, kuvuta maji salama na hata kuweka lami barabara zao.
Kule Lindi na Mtwara zao la korosho lilipo shamiri na wakulima kuanza kuhesabu milioni na ushee za mauzo, wengi walianza kuboresha makazi yao. Nyumba za udongo zilibadilishwa kuwa za saruji na kuezekwa kwa mabati.
2025 CCM mtatuambia nini ambacho hatujawahi kukisikia?