Salaam.
Kila anayefuatilia masuala yahusuyo siasa atakubaliana nami kwamba katika mkoa wa Mtwara, jimbo la Tandahimba ndilo linaongoza kwa siasa za upinzani.
Katika uchaguzi mkuu uliopita CCM walilikomboa jimbo hili toka mikononi mwa CUF ambapo mbunge aliyeshinda uchaguzi mkuu wa 2015 alitokana na chama hiki wakati katika ngazi ya halmashauri, chama hiki kilijizolea viti 27 kati ya 32 vya udiwani.
Licha ya CCM kulirejesha jimbo hili mikononi mwake katika uchaguzi mkuu uliopita kwa kujipatia mbunge na madiwani 31 kati ya 32, bado upinzani una wafuasi wengi sana katika jimbo hili. Katika siku za hivi karibuni hasa kuanzia kipindi yalipofanyika mabadiliko ya mkuu wa wilaya ambapo Rais Samia alimhamisha Bw. Sebastian Waryuba na nafasi yake kuchukuliwa na Col. Patrick Sawala aliyetokea wilaya ya Rufiji wananchi wanapitia wakati mgumu sana.
Baada tu ya ujio wa mkuu huyu mpya wa wilaya chuki ya wananchi dhidi ya Chama cha Mapinduzi na serikali yake imeongezeka mara dufu na hivyo kuupa upinzani turufu ya kushinda uchaguzi 2025. Licha ya kadhia nyingi zinazowapata wananchi, lakini hii ya askari wa jeshi la Polisi kuzunguka vijijini na kwenye mitaa ya mji wa Tandahimba wakikamata pikipiki hata zilizopo kwenye matengenezo inazidi kuichonganisha serikali na wananchi wake huku ikizidisha chuki ya wananchi dhidi ya chama tawala.
Askari wa jeshi la Polisi wa hapa wilayani hawana kazi nyingine wanayofanya zaidi ya hii ya kukamata mapikipiki mitaani na vijijini. Kwa hapa Tandahimba, kila askari yuko kwenye kitengo cha Usalama Barabani. Ukamataji huu hufanyika siku saba za wiki kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Huwa wanajaa kwenye magari mawili madogo ( Landcruiser) na huambatana na lori ya polisi ambayo hutumika kuzibeba pikipiki na kuzifikisha kituoni.
Ikumbukwe kwamba katika wilaya ya Tandahimba, 85% ya wakazi wenye umri unaoanzia miaka 25 wanamiliki pikipiki. Hapa Tandahimba pikipiki ni nyingi kama ilivyo kwa manispaa ya Shinyanga inayoongoza kwa kuwa na baiskeli nyingi. Kutokana na wingi huu wa pikipiki, viongozi wa jeshi la polisi wakishirikiana na mkuu wa wilaya wameamua kutumia hii kamatakamata kuwa mtaji wa kujipatia fedha kwa manufaa binafsi. Kuna OCD anaitwa Tesha. Huyu ndiye "master plan" wa mchongo huu. Huyu ndiye huruhusu wale askari kuendesha hii operation isiyo na kikomo. Na ndiye anayemfikishia DC fungu lake.
Kwanini wananchi wanalalamikia utaratibu huu unaokiuka haki? Ni kutokana na sababu zifuatazo:
i. Ukamataji huu haufanyiki barabarani badala yake askari huzunguka mitaani na vijijini na hukamata pikipiki hata zilizopo kwa mafundi. Pia huwa wanajificha vichochoroni hasa kwenye barabara za kuelekea maeneo ya vijijini.
ii. Asilimia kubwa ya wamiliki wa pikipiki hizo hulipishwa faini pasipo kupatiwa risiti za EFD badala yake huwapatia risiti za kuandika kwa mkono (hapa serikali inapoteza mapato yake).
iii. Kuna wengine hulipishwa faini ya Tsh. 30,000 kwa kila kosa na wanapohoji juu ya viwango hivyo vilivyofutwa na serikali kupitia bunge letu tukufu, hujitetea kwamba hawajaletewa waraka unaowaelekeza kutoza viwango vya sasa (Tsh. 10,000 kwa kila kosa).
iv. Ukamataji huu huendana na vipigo kwa waendesha pikipiki hao hasa kwa vijana.
v. Utendaji kazi wao hauzingatii idara mbalimbali zilizowekwa kisheria kwenye jeshi hilo kama vile Idara ya Usalama Barabarani, Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai n.k. Askari wote hufanya kazi moja ya kukamata pikipiki mitaani.
vi. Kadhia hii ipo hapa Tandahimba pekee tofauti na ilivyo kwenye halmashauri au hata miji jirani kama Nanyamba, Newala, Masasi na hata Mtwara Manispaa.
vi. Biashara zinadorora hapa mjini kwa kuwa wateja walio wengi toka vijijini wanasita kuja mjini kwa kuhofia kukamatwa. Badala yake wanasafiri kwenda miji jirani kama Newala ambako hufanya manunuzi ya mahitaji yao bila bugudha ya askari Polisi.
vii. Makosa yaliyo mengi yanatozwa faini ni ya kubambika kwani wakishakutajia hayo makosa unatakiwa kulipa faini pasi kuhoji.
Mwisho kabisa nikuombe Rais Samia, mchunguze mkuu huyu wa wilaya na ikibainika kwamba ni kweli anashirikiana na askari hawa wasio waaminifu basi tengua uteuzi wake kwani anakuhujumu wewe binafsi, serikali yako pamoja na Chama cha Mapinduzi.
Ikikupendeza mwagize IGP Simon Sirro amshushe cheo huyu Kamanda wa Polisi wa Wilaya aitwaye Tesha. Huyu ni mla rushwa na hana maadili ya kiaskari.
Kama Mh. Rais hutayazingatia haya basi jiandae kulipoteza jimbo hili kwenye uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika 2025.