2025 mwaka wa jasho na damu

Strong25

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2021
Posts
394
Reaction score
834
2024 ulikuwa nimwaka mgumu sana kwangu, sijui wapi nilifeli maana kama ni kupambana nimepambana sana ila sijaona hatua nilizopiga zaidi yamaumivu tu.

Mwaka huu kama Mungu atanipa pumzi na afya njema basi nitahakikisha napambana mpaka tone la mwisho la jasho na damu

Kabla sijaharibu uzi kwa wale ambao mmetoboa maisha mna kipi cha kunishauri nini niache, nini nifanye, njia gani nipite, ipi nisipite maana 2024 nimefanya karibia kila kitu kilichopo ndani ya uwezo wangu ila nimeambulia patupu

Naombeni muongozo wazee wangu ili kijana wenu nifike huko nakotaka kufika
 
2024 umekuwa changamoto kwa wengi, 2025 ni mwaka wa ku push hard once more.
Nevergive up, ji promise yourself
 
Go back to your roots, usiisahau mizimu ya kwenu
 
hii comment yako imeniwazisha sana_hii comment inaongea mengi sana
Ikuwazishe kweli mdogo wangu ,haya mashimo tunayapenda Ila sio kila shimo uweke maji Kaka .

Mengine Yana mikosi na ujinga mwingi Ila Mimi siamini hayo lakini nasikia wanaulimwengu wanasema hivyo .

Fungua dunia mdogo wangu ,sema wewe ni nani ? Una nini mkononi na wapi unataka kwenda ili dunia ijue ikiwa 2025 unatakiwa kuwa wapi ?

Pole Sana ,kazana ndiyo ukubwa na ndiyo uanaume ,natamani niandike na kakingereza ili kuweka msisitizo Ila ndiyo hivyo tena Kaka yako ni form three B
 
hahaha tena B lenyewe ulikua unakaa siti zanyuma _bro nimekupata sana .ila hakuna kitu kinauma kama inafika mwisho wamwaka unaskia wenzio wanaongelea mambo waliofanya ukicheki ww bado upo Zero
 
Ongeza juhudi na maombi
 
Shida wachawi! Ndo maana wengi tulikimbilia kwa Yesu! Mtafute Mungu wewe mwenyewe na hepuka kitu kinaitwa dini! Dini ni taasisi za kimafya za wizi!
 
Kama unatabia ya kusubiria mwaka mpya ndipo uanze kupambana rasmi - You're not ready.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…