Tuna raslimali nyingi sana kama madini lakini vinatufaidisha kwa kiwango cha chini sana.Hatuna mitambo ya kuchimba madini hayo,hatuna vifaa vya kisasa kwa ajili ya kilimo,vyote tunaagiza nje,ila tuna vyuo vikuu vingi,pesa nyingi inawekezwa kwenye elimu,tunasoma degrii za manunuzi kwa kuwa kipaumbele chetu ni kununua na siyo kuzalisha.
Nani Rais yule atakayefikiri nje ya boksi na kuufuta kabisa mfumo huu wa elimu ya magharibi?
Tunasoma mambo mengi ya kipumbavu kupoteza muda tu ili miaka ya kuhitimu iwe mitatu,minne au mitano. Lakini ukweli ni kwamba wahitimu ni majanga matupu hawana vitu vya maana kabisa zaidi ya kuongeza misamiati ya fani walizosomea tu.
Dunia imebadilika sana.Kuna vitu vingi mtu anaweza kujisomea mwenyewe tu na akafanya mambo makubwa bila kutumia mfumo wa elimu tulio nao.Mfano kuna watu wamesoma coding bila kufanya mtihani hata mmoja unaosimamiwa na profesa.Wanajisimamia wenyewe katika miradi wanayofanyia majaribio na wanafikia hadi kuwa wabobevu.
Kuna umuhimu wa kufumua kabisa mfumo wa elimu kwa kuanza na wasimamizi wa mfumo huu.Wote wapewe mtihani kueleza ni jinsi gani tutatatua changamoto zetu kwa kubadili aina hii ya mfumo wa elimu.Najua wengi wataandika siasa.Akiandika siasa afutwe kazi bila huruma maana hao ndio wanatuangusha.
Waletwe walimu kutoka China na wapewe nguvu ya kuleta nidhamu.Wanafunzi wanaoonesha uzembe wafukuzwe bila huruma. Tunahitaji Rais asiye mvivu wa kufikiri na anayechukia mambo ya siasa.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app