Namba 9 katika numerolojia ni namba ya mwisho Kwa sababu Kila namba katika maarifa hayo Inaweza kupunguzwa na kuwa dijiti moja. Inawezekana pia baadhi ya wataalamu kupunguza namba kuu "master numbers" kuwa dijiti moja.
1 mpaka 9 ndiyo uwanda wa numerolojia na mwaka huu 2025 ni sawa na 2+0+2+5
=4+5
=9
Namba zinapofika 9 katika numerolojia huanza kujirudia Kwa kuanza na 1 mfano 2026 itakuwa ni sawa na:
2+0+2+6
=4+6
=10
=1+0
=1
Maana yake ni kuwa namba zitaanza tena upya na kujirudia mpaka 9 na kuanza tena.
Kwa mantiki hii basi, kama maisha yanaweza kupunguzwa na kuwa namba ni dhahiri mambo mengi tunayoyafanya 2025 yapo mwishoni Ili kuanza upya.