21st to remember. Tarehe 21 ya kukumbukwa.. A count down!

Sioni hilo vumbi mpaka sasa
 
Copy & Paste from Setfree

Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hajatokea. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Kwanini Lopelope hajatokea?”

Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)

Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.

Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.

Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua atawanyakua wote waliotubu dhambi zao na kumwamini, na kuwapeleka mbinguni.

Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tujiweke tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; na dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.


Copy & Paste from Setfree
 
Unakopi na ku paste mada za wagonjwa wa akili ...rubbish kabisa. Maninah
 
 
Leo Polepole umesema jambo kubwa sana la namna kura zinavyochakachuliwa kimifumo. Integration ya mfumo wa CCM, Tume ya uchaguzi na NIDA ndo DUDE la kuibia kura.

Bila kubomolewa lile DUDE, CCM itatawala miaka 200 ijayo.

Ni ukweli ulio kweli kabisa, huku wana-ccm na wananchi tunaombwa kitambulisho cha Taifa (NIDA). Siku ya uchaguzi ni formalities tu, kura zinakuwa standby kusubiri minor adjustment kwenye mfumo ili watangaze mshindi.

Bila kupata wataalamu wa mifumo kutoka nje kwa ajili ya kufanya "Penetration Test" au "Systems Audit" kwenye DUDE kura ya mwananchi ni kama karatasi ya kuchambia haina thamani.

Wakikagua watu wa IT wa ndani baada ya zoezi wajiandae kuuma meno. Auditors lazima wawe na ulinzi wa taifa la nje na wakimaliza kazi zao wanatoa matokeo wanarudi zao kwao.

Polepole nimemsamehe madhambi yake yote kwa leo kuusema ukweli huu mchana kweupe. Naamini hata mbingu zitamsamehe. Maana amegusa kwenye afya ya Taifa juu ya haki
 
kwa mantiki hii hakuna haja ya kupiga kura.
na kumbe ndiyo maana viongozi wengi wa kuchaguliwa hasa wa chama tawala wanatuvimbia sana raia hadi kutuita kenge kwa sababu wanajua hatuna mchango wowote kwa wao kuwepo kwenye nafasi zao.
 
kwa mantiki hii hakuna haja ya kupiga kura.
na kumbe ndiyo maana biongozi wengi wa kuchaguliwa hasa wa chama tawala wanatuvimbia sana raia hadi kutuita kenge kwa sababu wanajua hatuna mchango wowote kwa wao kuwepo kwenye nafasi zao.
Bila hilo DUDE alilolianika Polepole kuondolewa au kufumuliwa kwenda kupiga kura wataenda wale makondoo na mambuzi. Wanaojitambua wasio wanufaika hawezi kupiga kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…