24/7 Huduma Usiku na Mchana Wiki Nzima

24/7 Huduma Usiku na Mchana Wiki Nzima

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Hivi pana sheria yoyote inayozuia biashara kufanyika usiku na mchana, siku saba kwa wiki (24/7) hapa Tanzania? Ni kwa nini basi biashara hizo hufungwa mapema, wakati wale waliokuwa maofisini wanapotoka na kuwa na muda wa kufanya manunuzi (jioni hadi usiku) au siku wanapobaki nyumbani (wikiendi na sikukuu)?

Nchi nyingine biashara ni usiku na mchana, wikiendi hadi sikukuu.

Kwa Tanzania nimeona sheli chache, na vituo baadhi vya kuziba pancha vikitoa huduma 24/7.

Tuanze na Kariakoo, na "Malls" zilizoko miji mikubwa Tanzania, kwa nini biashara zinafungwa zikiwa "anti-phase" na baadhi ya wateja, hususan wa maofisini? Kwa nini zisiwe 24/7?

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom