24 Hours of Le Mans: Shindano la Magari linalodumu kwa Masaa 24!

24 Hours of Le Mans: Shindano la Magari linalodumu kwa Masaa 24!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kwema wakuu?

Kuna hili shindano la magari linalofanyika kila mwaka mwezi wa sita katika mji wa Le Mans, Ufaransa, linaitwa "24 Hours of Le Mans".
images (8).jpeg

Hili shindano linakua nas magari sitini (60), ila yanagawanywa katika classes kama nne (4) hivi kutokana na performance, technology na aina ya gari, ila wote mna-race kwa pamoja ila kila class itakua na mshindi wake na pia kutakua na mshindi wa jumla.

Mashindano yenyewe:

Kama jina linavyojieleza, hapa tunaangalia gari ambayo mwisho wa masaa 24 litakua lime-cover distance kubwa kuliko wenzie.

Kwahiyo, tunataka tuone ni nani anatengeneza sport car, ambayo sio tu ina speed ila pia inaweza kuvumilia moto muda mrefu, pia ni fuel efficient na reliable.

Mnavyorace utakua na team itakayokusaidia kuweka mafuta, kufanya maintenance, kubadirisha oil au coolant etc.

Kuna siku za testing, na qualifications (grid) kama kwenye F1 ya FIA. Na nnavyoongea hapa kuna watu wanashindana.

Uwanja yanapofanyika

Kama tulivyosema mwanzo, mashindano yanafanyika mara moja kwa mwaka, mwezi June katika mji wa Le Mans Ufaransa, katika "Circuit des 24 Heures du Mans"

images (2).jpeg


Ni circuit ndefu yenye kilometa 13.6 ilioanza kutumika tokea 1923. Hii circuit inaunganisha barabara za mtaani na "circuit" za kutengenezwa.
images (17).jpeg

images (16).jpeg

Juu pichani ni Mercedes Benz CLR, mwaka 1999 ilipaishwa na Dumbreak akiwa katika race. Effect ya aerodynamics iyo.

Katika hii circuit kuna sehemu ni pamenyooka kwa kilometa 6 wenyewe wanapaita Mulsanne Straight, na ndio sehemu ambapo madereva wanafikaga hadi 407 km/h imagine, na mnatembea bampa to bampa. Hii sehemu madereva wengi sana wamefariki kwa ajali.
images (7).jpeg

Jumla ya kilometa zinazopigwa kwa iyo siku moja ni Kilometa 5,000 hadi 5,500. Au kwa wazee wa kusafiri ni sawa na kutoka Dar hadi Mwanza mara 5.

Magari yanayotumika

Kama tulivyosema, magari yamewekwa kwenye classes. Nitajaribu kuweka kwa kiurahisi izo classes.

Hypercar (H)

Haya yanakuaga 5 hadi 10 kutegemea na washiriki wa huo mwaka.
images (10).jpeg

Haya ndio top-class, ni magari yalio fast na yenye technology ya juu zaidi, mengine yanakuaga hybrids ana mengine ya kawaida. Na mara nyingi pia, yanakua designed kwaajili ya hizi "endurance" racing.
2024_6_Hours_of_Spa-Francorchamps_Toyota_Gazoo_Racing_Toyota_GR010_Hybrid_No.8_(DSC04184).jpg

Mfano: Toyota GR010 Hybrid (pichani hapo juu) Glickenhaus 007 LMH.

Hivi vigari vinakuaga na muonekano m-baya kwasababu ya kupambana na aerodynamics.

LMP2 (Le Mans Prototype 2)

Haya yanaweza kua 20 hadi 25. Yenyewe kidogo yamepungua nguvu ukifananisha na Hypercars, ila usiyachukulie ivyo.
images (11).jpeg

So kama jina lilivyo, yenyewe ni prototype cars yalivuokua yanadizainiwa na kutengezwa lengo ni kupunguza gharama ukifananisha na wenzao Hyper.
2022_24_Hours_of_Le_Mans_(52175732218).png

Mfano: Oreca 07 (pichani juu), Ligier JS P217.

LMGTE Pro (Le Mans Grand Touring Endurance Professional)

Haya yanaweza kua 8 hadi 12 kwa idadi. Mengi (au yote) kama jina linavyosema ni magari haya haya ya mitaani ila yaliyokua modified.
Porsche_GT_Team's_Porsche_911_RSR_at_the_2020_6_Hours_of_Road_Atlanta.jpg

Kwa kuyaangalia, yanafanana na magari ambayo tunapishana nayo siku zote sema ndio ivyo yapo modified na yanaendeshwa na ma-pro.
1280px-AF_Corse_Ferrari_488_GTE_Rigon_Silverstone_2018.jpg


Mfano: Porsche 911 RSR, Ferrari 488 GTE.

LMGTE Am (Le Mans Grand Touring Endurance Amateur)

Kama yalivyo aya hapo juu, LMGTE Pro, ila haya yanaendeshwa na professional na "amateur" drivers kama mimi na wewe.
1280px-PLM_2011_60_Aston_Martin.jpg

Magari aya hapa kidogo ni ya miaka ya nyuma ukifananisha na ya LMGTE pro.

Hapa yanakuaga magari 13 hadi 18.
DSC8983_(51577943248).jpg

Mfano: Aston Martin Vantage AMR, Chevrolet Corvette C8.R.

Utajiuliza, izo classes zina utofauti gani?


Speed na Technology:

Hypercars yenyewe yapo kibati kama tulivyosema kuliko wote, na yana technology ya hali ya juu, yakifuatiwa na LMP2, kisha LMGTE Pro, na mwisho LMGTE Am.

Class ya magari ya Prototype (wakina Hypercar and LMP2) yenyewe yalitengenezwa kama race cars, wakati izo GT classes (LMGTE Pro na Am) zilitengenezwa kama production cars, sema ndio ivyo ziko modified.

Madereva:

Tofauti nyingine ya hayo magari ni madereva wanayoyaendesha.
24_Hours_of_Le_Mans_2018_drivers_(28896068288).jpg

LMGTE Am zinaendeshwa na amateur drivers, wakati classes zingine wanaendesha ma-pro.

Ila kumbuka, classes zote tunaendesha muda mmoja na kwenye track moja.

Kwahiyo tegemea kutakua na overtaking za kutosha na a lot of fun.

Kila gari linakua na madereva watatu, wanaobadirishana zamu zamu na dereva hautakiwi kuendesha zaidi ya masaa manne straight na wala mwisho wa race usiwe umezidisha masaa 14 jumla. Mwenzio akiwa anakiwasha wewe unarest au unalala kabisa.

Mshindi

Kunakuaga na washindi wa aina mbalimbali. Ila tofauti na lengo la mashindano mengine ya magari kuangalia speed, hii wanalenga sana endurance kama tulivyosema mwanzo.
images (18).jpeg

Hii ni madereva wa Toyota walioshinda 2021.
Kwanza ni Mshindi wa Jumla.

Huyu ni mshindi aliekamilisha lap nyingi kuliko wote (kutoka classes zote), yes umekisia sawa, lazima atatoka Hypercars.


Pili, tuna Mshindi wa Class

Nadhani inajieleza, kwamba katika class zetu nne, kila moja inatoa mkali wake.


Kwa mfano, Mwaka 2023 mshindi wa 24 Hours of Le Mans alikua Ferrari AF Corse team walikua na gari lao namba 51, Ferrari 499P Hypercar.
Ferrari_499P_-_Hybrid,_2023.jpg


Madereva watatu walikua
Alessandro, Calado, na Antonio.
images (15).jpeg


Washindi kw ujumla walikua hivi:
images (19).jpeg



Mwaka 2024 unaangalia?
images (9).jpeg

Kuna mabadiriko kidogo kwenye classes za mwaka huu ila haitatoka kwenye general niliokuambia hapo juu. Mwaka huu tuna:

Hypercar Class (LMH and LMDh) tutawaona Toyota, Ferrari, Porsche na Lamborghini watakuja na SC63 na BMW watakuja na V8 yao hybrid.
images (13).jpeg

Kusema kweli BM muonekano wake dah. Sema sawa.

images (14).jpeg

Bwana kuna hawa wageni Isotta Fraschini ali-perfom vizuri sana juzi kwenye mazoezi, alitokea nyuma ila akawaonyesha wakongwe kazi.


LMP2 Class inakuaga competitive sana, kutakua na magari 16 yakiwemo 6 ya Pro-Am.


GT Class (LMGT3) ni kama class mpya kaa matamshi au muandiko ila ndio ile GT ya production cars. Watakuepo 23 kutoka makampuni kama Aston Martin, Corvette (ko-ve-te), Ferrari uwa anaweka pia, BMW, Lexus, McLaren.
images (12).jpeg

Hii class inakuaga tamu kwasababu ni gari ambazo ukiotea hela unaweza kununua.

Race itaanza Jumamosi hii tarehe 15 saa 11 jioni masaa ya Africa Mashariki na itaisha muda huo huo kesho yake jumapili.


Movie:

Kuna movie inaitwa Gran Turismo, ya 2023 kidogo ukiicheki unaweza kuoata fleva ya hii race walirace muda mwingi wa movie.
images (6).jpeg

Unaweza itafuta kama mtu wa movie.

PS: Wazee wa pikipiki nao wana Le Mans Motorcycles. Ni fire nayo.

Pamoja sana.
 

Attachments

  • images (16).jpeg
    images (16).jpeg
    23.5 KB · Views: 9
  • images (11).jpeg
    images (11).jpeg
    36 KB · Views: 11
Aaah, mkuu umeshusha vitu vitamu sana, kiufupi hii race hua ni balaa na hizo hyper cars na classes nyingine wamezio geza ili kuzidi kunogesha mashindano but original yalikua ni Gt tu.

Humu kulikua na unyama wa kila aina na fauls za kutosha. Kwa mtu wa movies pia fuatilia movie inaitwa Ford vs Ferrari, humo utauona unyama wa ford Gt40.
 

Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    30.9 KB · Views: 11
Aaah, mkuu umeshusha vitu vitamu sana, kiufupi hii race hua ni balaa na hizo hyper cars na classes nyingine wamezio geza ili kuzidi kunogesha mashindano but original yalikua ni Gt tu.

Humu kulikua na unyama wa kila aina na fauls za kutosha. Kwa mtu wa movies pia fuatilia movie inaitwa Ford vs Ferrari, humo utauona unyama wa ford Gt40.
Dah weekend hii nitakua sina maisha nataka nitafute bundle nitulie ghetto nafuatilia. Mwanzoni na mwishoni inakuaga tamu sana.
 
Dah weekend hii nitakua sina maisha nataka nitafute bundle nitulie ghetto nafuatilia. Mwanzoni na mwishoni inakuaga tamu sana.
Unyama utakua ni mwingi sana mkuu, ngoja tuone itakavyokua.

Kama huto jali ukipata muda Shusha uzi wa Rally ni moja kati ya kitu tamu sana katika mashindano ya magari. Pia mtu anaweza kwenda shuhudia live hapo kenya kila mwaka.
 
Unyama utakua ni mwingi sana mkuu, ngoja tuone itakavyokua.

Kama huto jali ukipata muda Shusha uzi wa Rally ni moja kati ya kitu tamu sana katika mashindano ya magari. Pia mtu anaweza kwenda shuhudia live hapo kenya kila mwaka.
WRC yeah. Ngoja weekend hii nitaiandaa. Mtu ukijipanga unaenda KE chap tu.
 
Cardillac watakaa nafasi ya pili na tatu (wana magari mengi)

Bwana Ferrari ambae mwaka jana alikua mshindi, atakua nafasi ya 4 na 5 atakua Alpine (branch ya BMW)
 
Halafu kuwekwa kwenye mstari wa mwisho unachagua au unachaguliwa?
Mnafanya Qualifying. Wanawapa mfanye mashindano against time. Aliefast anakua wa kwanza na alie slow anakua wa mwisho.

Yaani mfano mechi si Kesho jumamosi, sasa jana Alhamis wamefanya Qualy ambayo ndio itachagua nani akae wa kwanza na nani akae wa pili, hadi wa mwisho.

Kwahiyo kwa kufuata classes za magari, Hyper wana formation zao (wa kwanza hadi wa mwisho, kisha class ya LMP2 nayo ivo ivo, hafu LMGT3 nayo hivo hivo.

Class ya magdri yaliyo slow (LMGT3) ndio inakua mbele, hafu class ya fast Hyper zinakua nyuma.

Yaani mwendo wa kuovertake tu.
 
Back
Top Bottom