2pac na chimbuko la uanaharakati wake kudai haki

mwandorobo

Member
Joined
Jul 7, 2018
Posts
17
Reaction score
20
Habari za muda huu, nilitaka ku share kidogo ka stori ka mwanaharakati huyu kupitia muziki wa rap.

Tupac Amaru Shakur alizaliwa mnamo mwezi kama huu tarehe 16 mwaka 1971, ikiwa leo hii tumebakiza siku nne tu kuadhimisha kuzaliwa kwake.

Historia ya harakati za 2pac inaanzia tangu akiwa tumboni mwa mama yake Afeni Shakur ambaye alikuwa ni mwanaharakati wa chama cha The black panthers.

The black panther s ni chama kilichokuwa kikitetea haki za watu weusi zilizokuwa zinaminywa kutokana na ubaguzi wa rangi katika Marekani.

Hivyo basi tunaona 2pac anazaliwa na kukua katika mazingira ambayo mama yake na nduguze waliomzunguka wote wamo ndani ya black panther party.

Ingawa 2pac alikulia katika mazingira magumu ya kifedha mama yake akiwa ni mtumiaji wa cocaine, 2pac alijihusisha na vitendo vya uhalifu pamoja na kuuza dawa za kulevya akiwa kijana mdogo na ndio maana ukisikiliza nyimbo zake nyingi amekuwa akiimba kuhusu maisha yake halisi ya uhalifu (life of crime) na kupelekea kujiita thug na kutengeneza thuglife tattoo mwilini mwake.

2pac amekuwa akitetea haki za watu weusi kupitia mashairi yake ambayo amekuwa akiyaunganisha moja kwa moja na maisha yake halisi katika utafutaji wa maisha mazuri mtaani.

Mfano wa wimbo wa "I wonder if heaven got ghetto" 2pac ameimba akijifanyia tathmini iwapo kutakuwa na maisha mazuri kwa watu wa jamii yake ambao dunia inawaona kama ni wahalifu tu na watu wa chini ambao hawastahili jambo zuri lolote katika nchi yao.

Pia katika wimbo huo ameongelea jinsi Marekani illivyokuwa haiko tayari kuwa na Rais mweusi.

Uhalifu, Police brutality, mauaji, unyanyasaji wa kijamii ni vitu ambavyo 2pac amekuwa akiviimba sana kwenye nyimbo zake.

Thread ijayo nitachambua wimbo mmoja baada ya mmoja wa 2pac Shakur ili tuweze kuona kiundani ni kwa namna gani 2pac alikuwa ni kama mkombozi mweusi (black jesus) kama wengi wanavyosema kupitia mashairi ya nyimbo zake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…