Film za 3D ukiziangalia ni kama vile wamepiga picha katika layer nyingi na kuziweka pamoja. Ukivaa miwani, zile layer zinatenganishwa na kuna layer zinakuwa zimesogezwa karibu na muangaliaji. Usipovaa miwani unaziona kabisa kama picha zimelaliana.
Ukiangalia kwenye screen, unaona kama vile vitu vinaanzia kwenye screen na kwenda nyuma yake (vile vilivyo mbali). Kwenye 3D, picha zinakuwa pia zimesogezwa pia kwa mbele, kwenye screen na za nyuma.
Nakubaliana na mkuu hapo juu kuwa nenda mwenyewe kwenye majumba ya cinema ili uweze kushuhudia hiyo hali vinginevyo hutaweza kushuhudia hii hali. Kama uko Tanzania basi kuwa na subira maana muda si mrefu, TV au screen za 3D zitaingia hadi huko ingawa zinaweza kuwa ni zile za kutumia miwani.
Ila kumbuka kuwa kama una matatizo ya macho, unaweza hii kitu usiione maana inakuwa kama unadanganya macho ya kawaida na kuna wengine ambao wanavaa miwani na kwa maana hiyo hawana ya kawaida, huwa wanalalamika macho kuuma au kutokuona. Nafikiri inabidi avae miwani yake na hiyo PORALISED. Ndiyo maana miwani PORALISED ukiangalia kwenye saa zile za kukonyeza, huoni kitu?? (sina uhakika ila kuna kitu hakiko sawa).
Miaka hiyoo nilibahatika kwenda kuangalia kwenye Imax na kwenye film kulikuwa na lijimjusi linaogelea majini. Mkia wake ulikuwa kama vile unapita mbele yangu. Nilitamani ninyenyue mkono na nimguse ingawa ukweli ni kuwa alikuwa mbaali saana (screen). Jaribu kuangalia hizi picha, na angalia kwenye Youtube utaona monitor za 3D na miwani yake.
http://arstechnica.com/gadgets/news/2010/01/3d-tv-is-coming-ready-or-not.ars
Sijui kama hii kitu itakusaidia sana ila ukweli ni kuwa unapoangalia kama mpira wa miguu, unakuwa kama vile na wewe unacheza. Nafikiri unaweza hata ukaruka upige tick tack.......
Hii kitu unaweza kuiona kama unaangalia mpira uliopigwa na kuilenga camera. Unaruka au kufumba macho kwani unapata feeling kwamba unakuja kukupiga machoni.