BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwenyekiti wa Mtandao wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Prof. Andrew Swai, ameyataja baadhi yanayosumbua Watu wengi kuwa ni pamoja na #Kisukari, #Saratani, Magonjwa ya #Akili, #Figo, #Macho na Shirikizo la Damu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Prof. Paschal Rugajo, sababu kuu za kuongezeka kwa Magonjwa hayo ni pamoja na Wananchi kupuuza Ushauri wa Wataalamu kuhusu kubadili Mtindo wa Maisha hasa #LisheBora na #Mazoezi.
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha mwaka 2017 Magonjwa Yasiyoambukiza yalichangia Vifo 134,600 sawa na 33% ya Vifo vyote vilivyotokea. Aidha, gharama zilizolipwa na NHIF kwa Magonjwa hayo zikifikia Tsh. Bilioni 99.09 kwa mwaka 2021/22.