Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Nyanja: Demokrasia
Jenga urafiki na mtu aliyeko ndani yako, mpatane, ili uhojiane naye kwa sababu anakufahamu fika, usihojiane na mtu aliyeko nje yako ambaye hawezi kukupa uhalisia wako maana hakujui vizuri, (ndani yako kuna mtu pia usiyemwona kwa macho yako lakini anaishi na anaratibu maisha yako mazima, huyu mtu ni wewe halisi, hivyo mko wawili katika moja (two in one), mpe nafasi, msikilize, usimpuuze eti kwa kuwa humwoni kwa macho yako).
Muulize huyo mtu aliyeko ndani yako kuwa kama ungekuwa rais ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Mhe. Rais SSH?, Je, ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Mhe. Dkt. Magufuli kwa spidi na muda mfupi namna ile? Je, ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Mhe. Jakaya Kikwete? Je, ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Mhe. Ben Mkapa (Big Ben)? Je, ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Baba wa taifa Mwl. JK Nyerere? Je, ungeifanyia nini Tanzania kuliko alichofanya Mhe. Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine mwaka 1984 (rejea hotuba ya Mwl. Nyerere ya Aprili 8, 1983 kuhusu vita ya uchumi wa taifa)?
Utajiri wa nchi kama hakuna mfumo imara wenye tija wa kupatikana viongozi bora; wakati fulani unaweza kuiingiza kwenye matatizo makubwa yanayosahihishika kwa gharama kubwa ya rasilimali na muda yatokanayo na watu kusukumwa kutanguliza uchu badala ya sifa-stahiki za kuwania madaraka ya kuongoza nchi, uchu ambao msingi wake ni tamaa kali (lust) ya rasilimali zinazotengeneza utajiri wa nchi, hili ndilo tatizo linalozitesa na kuziseta nchi za Afrika zikiwemo Nigeria, Comoro, DR Congo, hata na Afrika Kusini ambayo ni demokrasia kongwe barani Afrika lakini viongozi wake ukiachilia muasisi wake Rais Mandela wamekuwa hawamalizi awamu zao za uongozi bali wanakatishwa katikati ya safari kwa siasa chafu (junk politics) za wenye uchu wa urais kwa nia ovu ya kumiliki ukwasi kupitia rasilimali za nchi. Tanzania inatajwa kuwa ni ya pili duniani kwa utajiri wa vivutio vya utalii nyuma ya Brazil, ukiachilia rasilimali zingine lukuki.
Nafasi ya urais ni nyeti sana, haihitaji kupatikana kwa bahati nasibu wala kwa zamu, rais hawezi kuwa zaidi ya mmoja kama walivyo Wabunge na Madiwani katika awamu moja. Vigezo vilivyotumika kuchagua sifa hizo kwenye jedwali hapo chini ni tunu za taifa, mambo ya msingi katika malengo ya Dira ya Taifa 2025 na falsafa ya nchi ambavyo hivi ndivyo vinashughulika na mustakabali wa taifa. Aidha, vigezo hivi siyo Alfa na Omega.
Weka alama ya tiki/vema kwenye kisanduku cha ama NINAWEZA au SIWEZI mbele ya kila sifa na vielelezo vyake alafu jisahihishie mwenyewe uone matokeo ambayo pia yatakuonyesha kama unatosha kuwa rais wa Tanzania kwa wakati wo wote ule baada ya Mhe. Rais SSH kuhitimisha awamu yake kwa mujibu wa katiba ya nchi. Ukipata alama nyingi za NINAWEZA basi unaweza kujiwazia kuwa na sifa za sekondari (siyo za msingi) za kutia nia ya kazi ya urais. Ukipata alama nyingi za SIWEZI basi waweza kufikiria kazi nyingine zaidi ya hii ya urais ambayo kiwango cha ugumu wake kinaweza kuelezewa vizuri na mfano wa utitiri kumbeba tembo. Baba wa taifa Mwl. JK Nyerere aliwahi kuwakemea wenye uchu wa kwenda ikulu kwa kuwaambia kwamba ikulu ni mzigo, mwandishi anakubaliana na kauli hii ya Baba wa taifa; kwa kutumia istilahi za sanaa-ya-lugha kuwa ikulu ni sawa na kulalia kitanda chenye kunguni wengi.
Wanasaikolojia wanaamini kuna uhusiano wa karibu kati ya tabia fulani na hatia Melgosa et al, (2017). Itoshe ujitathmini kama tabia zako kwenye hizi sifa ikiwa utakuwa rais zitasababisha hatia au usalama.
Jitathmini kwenye jedwali hapo chini kama ungekuwa rais ungeifanyia nini Tanzania (tathmini hii siyo rasmi kiserikali, kichama na makundi maslahi mengine yote)
Naomba kura zote.

S/N | SIFA | VIELELEZO | NINAWEZA | SIWEZI |
1 | Rekodi ya uadilifu | Kuheshimu viapo, kuepuka maslahi binafsi kwenye masuala ya umma, uwezo wa kudhibiti uchu-binafsi wa mali na madaraka, uimarishaji maadili ya kitaifa. | | |
2 | Kulinda rasilimali za taifa | Ulinzi wa maliasili, utokomezaji ujangili na uharamia kwenye hifadhi za taifa za nchi kavu na majini ikiwemo uvuvi haramu, kudhibiti utoroshaji madini na makinikia nje ya nchi, maboresho makubwa ya sekta ya ardhi kutokomeza ukabaila mpya uliovamia nchi, uainishaji upya wa mipaka ya JMT na ile ya ndani, utunzaji mazingira (Green-Politics), kuhakikisha matumizi mazuri ndani ya serikali, ndani ya vyama vya siasa na asasi za kiraia. | | |
3 | Kicho cha Mungu | Kutolifitini taifa, kuepuka ukibaraka (uwakala wa ubeberu), kulaani uchochezi wa machafuko, kutokuwa na hisia za udini, kuepuka ubaguzi wa aia zote, kuwa mtu wa ibada, kuwaenzi viongozi wakuu wa kitaifa wastaafu (waheshimiwa marais na wake zao, waheshimiwa makamu wa rais, waheshimiwa mawaziri wakuu, waheshimiwa wakuu wa mihimili ya Bunge na Mahakama i.e. maspika na majaji wakuu wakiwemo wakuu wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama). | | |
4 | Kupambana na rushwa na ufisadi | Kukana undugunaizesheni katika kuviondoa, kusimamia usafi wa chama na serikali, kuimarisha taasisi za kupambana na rushwa na ufisadi, kupunguza rushwa ndani ya taasisi za kutoa huduma, haki na ajira, kupunguza rushwa ya uchaguzi ndani ya serikali na ndani ya vyama, kuishi kwa kiasi, utayari wa kustaafu urais bila kuwa na mapato ya aibu nje ya yale yaliyotamkwa na katiba ya taifa, ujasiri wa kukataa kupokea zawadi-binafsi zitokanazo na dhamana ya madaraka yako rasmi. | | |
5 | Ukusanyaji mapato | Uimarishaji taasisi za kodi, uzibaji mianya ya uvujaji na ukwepaji kodi, ongezeko la makusanyo, ongezeko la walipa kodi, ongezeko la hiari ya kulipa kodi bila shuruti, kupunguza rushwa kwenye ulipaji kodi, kupanua wigo wa utafiti wa masuala ya kodi, biashara na uchumi. | | |
6 | Kulinda, kuhifadhi na kuendeleza uhuru wa taifa | Kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama, kuendeleza urafiki (siyo fitna) na mataifa na taasisi za kimataifa, kushiriki utatuzi migogoro kwa majirani, ulinzi wa mipaka ya nchi angani, majini na nchi kavu, kuendeleza falsafa ya Tz ya siasa za kutofungamana na upande wo wote, kuendeleza, kulinda na kuhifadhi muungano wa Tanganyika na Zanzibar. | | |
7 | Kiwango cha uzalendo | Uongozi ni utumwa na utumishi kwa watu, siyo fursa ya kupata ukwasi Moringe et al, (1980s) nukuu isiyo rasmi. Kuipenda Tanzania, kuweka hazina binafsi ndani ya Tanzania badala ya offshore. | | |
8 | Kutoa na kusimamia haki | Kuepuka matumizi ya Kauli-gongana (Double Standards) katika kutoa na kusimamia haki, kutekeleza kivitendo kaulimbiu ya “rushwa ni adui wa haki” hutapokea wala kutoa rushwa. | | |
9 | Miundombinu na huduma za jamii | Kutotumia kigezo cha ukabila na ukanda, kuimarisha upatikanaji wake, kuepuka kutoa ahadi zisizotimia (Easier said than done) za ujenzi wa miundombinu na utoaji huduma za jamii. | | |
10 | Kuzuia maonevu kwa wanyonge | Uwezo na dhamira za kuhakikisha urejesho wa haki zilizodhulumiwa, mapambano dhidi ya janga la dawa hatari za kulevya, kulinda haki ya kuishi, kupambana na ukatili wa kijinsia, kuruzuku wanawake, watoto, vijana na watu wanaoishi na ulemavu, kuwaenzi wazee (In Australia, Poverty Report (1976) found that the problem of stigma against the aged pensioners as being among the poorest groups in the population was addressed), kuondoa uonevu kwenye vyombo vya dola dhidi ya raia wanyonge na maskini ili waufurahie uhuru wao kamili na kurejesha imani yao kwa vyombo vya dola (watu wema wasimkimbie askari bali wamkimbilie), kuondoa ukaburu wa wenye ukwasi na madaraka. | | |
11 | Kulinda na kuendeleza amani ya nchi (rejea aya ya 4 ya sura ya kwanza kupata maarifa kabla ya kujibu sifa hii) | Kuvutia mitaji, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kupunguza tofauti kubwa za viwango vya maisha, kuweka dhamana ya kiserikali kwa mahitaji ambayo yako nje ya uwezo wa wananchi kupatikana, kupunguza matukio ya ujambazi, kupunguza ajali katika vyombo vya usafiri, kuondoa migomo kwenye taasisi za mafunzo na zile za kazi ikiwemo sekta binafsi inayotoa huduma kwa umma. | | |
12 | Vitendo kuliko nadharia | Ujasiri, uthubutu na ubunifu, kutoyumba katika maamuzi, uwezo wa kuwakana ndugu na marafiki unapolinda maslahi ya umma haijalishi mnashabihiana kiitikadi, uwezo wa kufasiri nadharia kwenye vitendo, uwezo wa kusimamia michakato ya mabadiliko, tajiriba na ragba ya kuratibu dharura za kitaifa kwa tija kubwa (kwa kila dharura ndani yake kuna fursa yenye tija). | | |
13 | Uhuru wa mihimili | Kutoingilia maamuzi ya mihimili, kuzipa uwezo wa kibajeti wa kujiendesha kwenye masuala mbalimbali zikiwemo mafunzo, miundombinu, ajira na teuzi mpya, kuziwezesha kujielekeza kwenye malengo ya kitaifa ya Dira ya 2025, tunu za taifa na falsafa yake, kushirikiana kwa kushauriana kwenye masuala yenye maslahi mapana ya umma kwa ajili ya kujenga taifa moja imara lililoshikamana. | | |
14 | Utawala Bora na wa Sheria | Kuheshimu katiba ya nchi, uboreshaji sekta ya sheria na idara za mahakama na magereza, kutambua na kushirikiana na wadau wa utawala bora na wa sheria e.g. taasisi za kisheria na asasi za utawala bora na haki za binadamu. | | |
15 | Udhibiti wa sekta ya utumishi | Umakini wa uteuzi viongozi, ufuatiliaji viapo vya watumishi, sensa ya taifa ya watumishi wa umma kubaini idadi ya watumishi na viwango vya weledi, maboresho ya maslahi ya watumishi, usimamizi madhubuti wa sekta ya hifadhi za jamii hasa kwenye maeneo ya mafao, pensheni na bima za afya za watumishi. | | |
16 | Ukuzaji Demokrasia | Uwepo wa vyama vya siasa na asasi huru za kiraia, maamuzi kufikiwa kwa ridhaa ya wengi wa watu, uongozi kupatikana kwa uchaguzi siyo kwa mapinduzi ya serikali na ndani ya vyama, kuheshimu ukomo wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya taifa na za vyama. | | |
17 | Uimarishaji uhusiano wa kimataifa | Urejeshaji uhusiano wa kibalozi zikiwemo nchi za kimkakati, uimarishaji diplomasia ya uchumi, ufuatiliaji utendaji wa ofisi za kibalozi za Tz, uendelezaji wa uanachama katika taasisi za kimataifa na jumuiya za kikanda, upanuzi wigo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. | | |
18 | Ukuzaji uchumi wa taifa | Marejeo ya mikataba ya uwekezaji, kuimarisha biashara za wanyonge, mapitio upya ya sheria na sera ili kuhakikisha maslahi ya taifa, kuondoa uvamizi wa mabenki, kudhibiti utakatishaji wa fedha, kupunguza mfumuko wa bei, kudhibiti dolaraizesheni ya uchumi wa taifa, kuboresha thamani ya fedha ya taifa, kutekeleza Dira ya Taifa ya 2025, kupunguza umaskini kupitia ujenzi wa uchumi jumuishi (economic inclusion), kutekeleza mkakati wa kujadiliana na wafanyabiashara (Business Dialogue). | | |
19 | Kuimarisha sekta ya kilimo | Kushughulika na bei na tozo za mazao, uimarishaji bodi za mazao na uhuishaji vyama vya ushirika, ufufuaji wa mazao yalokuwa kwenye hatari ya kutoweka km mibuni, michikichi, mpira, mwani, vanila nk, dhamira ya kutokomeza njaa, ugavi wa pembejeo, utatuzi wa migogoro ya mipaka ya viwanja na mashamba, kurejesha mahusiano mazuri baina ya wakulima na wafugaji, dhamira ya kuanzisha skimu za umwagiliaji. | | |
20 | Ukuzaji sekta ya viwanda | Ufufuaji viwanda vya zamani, uanzishaji viwanda vipya vya kuchakata mazao ya kilimo na mifugo, viwanda vidogovidogo (Cottage Industries), viwanda vikubwa katika sekta isiyo rasmi. | | |
21 | Kuweka uwiano mzuri baina ya ugenishaji na uzawa (Foreignization vs indigenization) wa uchumi wa taifa (Hivi sasa nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na tatizo la ugenishaji mfano kwenye sekta ya utalii (na hata uvunaji wa madini na vito) sehemu kubwa ya mapato yanarudi nje ya Afrika, mfano ndege za kuleta watalii ni za kwao, makampuni ya kitalii (tour operators) ni ya kwao, hoteli za kitalii ni za kigeni au zinaendeshwa na wawekezaji wageni, vinywaji katika hoteli hizo zinaagizwa kutoka kwao, hivyo sehemu kubwa ya mapato inavushwa nje ya mipaka ya Afrika kuwarudia wao, Prof. Wangari Maathai), nukuu isiyo rasmi. | Kuboresha na kuimarisha taasisi za uwekezaji, kufufua miradi ya umma iliyohujumiwa na ile iliyowekwa chini ya ufilisi, kutoa vichocheo vya uwekezaji (investment incentives), kutoa hakimiliki kwa ardhi za kimila ambazo zinaweza kutumika katika uwekezaji mdogomdogo au hata kukodishwa kwa wawekezaji wakubwa (wageni na wazawa), kuruhusu wawakilishi wa ndani (local partners) wa uwekezaji wa kigeni, kuweka uwiano sahihi wa uwekezaji nchi nzima bila ubaguzi wa kijiografia. | | |
Jumla ya alama | | |
Naomba kura zote.
Upvote
0