Kwa sisi wenye interest na 3D designing njia mojawapo itakayotusaidia ni ushurikiano, ingawa sijui ni kwa namna gani kutokana na tofauti za kijiografia, lakini kwa mfano tunaweza kufanya mpango sisi ambao tuko tz tukafanya ka ushirikiano fulani, kwa mfano tukawa tunakutana mara mojamoja tukiwa na Laptop zetu, tukabadilishana software, mawazo nk, hii ni kutokana na kwamba hapa kwetu sidhani kama kuna shule za ukweli, wengi wetu tunajifunza out of passion na interest, kwa mpango huo sisi tutakuwa walimu na wanafunzi at the same time.
Niliwasiliana na mwana jf mwenzetu 3D. akasema tatizo la kujifunza bila mwalimu ni kwamba muda mwingi unatumika kuapat solution ya kitu ambacho mwalimu ange solve within a fraction of minutes. kwa hiyo tukifundishna wenyewe inaweza kusaidia kidogo.
Tukijitahidi watoto wetu wataacha kuangalia Tom & Jerry na wataangalia katuni za kiswahili za Sungura Mjanja, Juma na Roza, na pia tutatengeneza katuni zenye maudhui ya kwetu hata kama zitaongea kiingereza. Pia tutakuwa na satisfaction kwmba tume achieve goals zetu asikwambie mtu graphics ina raha yake bwana.
Good-luck all