4% ya mapato kwenda Zanzibar kama Hoja ya Muungano

20% inatoka kwenye mapato ya sehemu zipi????

Mapato ya TRA Zanzibar yanachukuliwa na serekali ya SMZ. Ila hayo mapato ya TRA Zanzibar hayazidi hata 20% ya stahiki ambayo SMT wanatakiwa kuilipa SMZ ya gawio la pato la Muungano. Na ndio mana SMZ wanadai hela zao.
 
Hiki ulichoandika hapa ni kituko, kwani Watanzania si ni wamoja? Hayo ni miongoni mwa makubaliano ambayo yapo kikatiba, Rais akitokea bara, Makamo wake atatokea visiwani na Rais akitokea visiwani Makamo wake atatokea bara.
Au ulitaka aje Mholanzi kuwa Rais wetu?
 

Kivipi ebu dadavua hoja yako.... Kwani kati ya Tanganyika na Zanzibar ipi yenye mapato makubwa?!!!
 
Actually ni vyema tungejua mchango wa Zanzibar katika Muungano na vitu vya Muungano na visivyo vya Muungano . Ili ijulikane zipi ni secta za watanganyika tuu na zipi ni za wazanzibar tuu. Hii ni katiba mbovu na imepitwa na wakati.
 
yaani Zanzibar ni nguzo ya utalii Tz? wewe upo tz ya wapi? zanzibar ngi nguzo ya utalii kuliko ngorongoro, serengeti, mikumbi na mbuga zote hizi? akili yako umetupa wapi?
Zanzibar haina kitu chochote cha kuizidi Tanganyika. Wenyewe kwenye utalii ni zile beach hawana kitu kingine. Beaches Tanganyika zipo nyingi Sana kwahiyo ni kuboresha tuu . Mwambao wa bahari kuanzia Tanga mpaka Mtwara . Visiwa na mwambao wa maziwa yote vya na visiwa vyote vya bahari ya Hindi mfano mafia na vya ziwa Nyasa , Tanganyika na ziwa Victorian
 
Bandari ya Zanzibar haitaweza kuizidi bandari ya Dar es salaam kwasababu Zanzibar ni kisiwa kidogo Chenye population ndogo ya watu. Tanganyika kuna watu takribani 60 Million Vs 1million Zanzibar na kuna nchi ambazo ni landlocked zinaitegemea Tanganyika. Haitawezekana mzigo uende bandari ya Zanzibar ndio uje bandari ya Dar. Hapo umechemsha.
 
ulitakiwa kusema, hata kama bandari ya zanzibar itakuwa huru still ni mizigo michache itabebwa pale kwa ndege kama itatakiwa kwenda landlocked countries za africa mashariki na sadc. kama mizigo hiyo itatakiwa kwenda huko lazima itatakiwa kupitia tena bandari ya dsm na itapigwa ushuru vilevile na itabebwa na malori au reli ya bongo vilevile. kwamaana hiyo, Bara ni mdau mkubwa sana wa uchumi wa Zanzibar na katu zenji wasijefikiri watafanikiwa wakijitenga na pengine kuwa adui wa bara. ni mawazo yao ambayo yapo kwenye makaratasi ila kwenye practice watakuja kujutia na hatutawapa nafasi hiyo tena kwasababu na sisi tutakuwa tumeonja utamu mpya.
 
Si mlisemaga kuwa watoto wa kike hujali sana wa nyumbani kwao au mi ndo sikuelewa sawasawa nini wajameni!?
 

Mkuu Zenj hawana mipango ya uadui na Bara, Zenj wanadai haki zao, Zenj wanadai uhuru wao. Sasa kudai haki zao na uhuru wao ni uadui ?
 

Mkuu unasahau tu kuwa Kuna Kenya na Msumbuji juu na chini ya bara. Tanganyika akisusa wenziwe watakula.
 

Mkuu turufu ya Zanzbar kwenye sera za biashara ni free port na free zones, Hiyo watapiga bao tu kivyovyote.
 
Kivipi ebu dadavua hoja yako.... Kwani kati ya Tanganyika na Zanzibar ipi yenye mapato makubwa?!!!
Kwa mujibu wa article of Union Bandari, Customs, Income tax ni Mambo ya Muungano. Kwa maneno mengine ni mali ya Tanzania (si Tanganyika peke yake wala Zanzibar peke yake ni mali ya ushirika).
Kumbuka Muungano huu si wakila kitu,ni baadhi ya Mambo tu.
Hivyo basi yale mambo ambayo si ya ushirika (MUUNGANO), Kila upande ugharamie kivyake vyake isitumie Pato la Ushirika. Pato la Ushirika litumike kwa Mambo ya Ushirika tu mfano ulinzi, Mambo ya ndani, Elimu ya Juu n.k sio kwenye Afya, Kilimo wala barabara na kama hayo yasiyo ya Muungano.
Jibu la hili ni AKAUNTI YA PAMOJA.
Sijui nimeeleweka?
 
Mkuu turufu ya Zanzbar kwenye sera za biashara ni free port na free zones, Hiyo watapiga bao tu kivyovyote.
Bandari ya Zanzibar itawasaidia wazanzibar wao tuu. Haitatusaidia Tanganyika kwasababu Tanganyika ina mwambao mkubwa kuizidi Zanzibar ina strategic zones za kujeng bandari mpya nyingi zaidi from Tanga to Mtwara + mafia Island. wala bandari ya Zanzibar haitawasaidia other landlocked countries especially in Zambia, Malawi, Zimbabwe, Burundi, DRC, Uganda na Rwanda. Ni ngumu kusema mzigo especially raw materials ( especially Mazao, madini , mafuta) uje bandari za Tanganyika ndio ukachukue meli nyingine uende Zanzibar ndio uende western countries au Asia. Lakini pia ukiangalia mizigo ikitoka china au Asia au other western countries uende Kwanza Zanzibar ndio uje Tanganyika halafu uende other landlocked countries. Tanganyika ipo kwenye strategic location. Pia Zanzibar hayo mafuta yanayoongelea ni ndoto za Alinacha hamna kitu kila mwaka mafuta mafuta . Lakini hayachimbwi. Hata ukiangalia kwenye nchi zilizogundulika kuwa na Mafuta Zanzibar/ Tanzania Haipo. Utaona tuu kuna gesi iliyogunduliwa ipo Mtwara na sehemu zingine za Tanganyika na madini mbalimbali yaliyopo Tanganyika tuu. Huruma za Mwl Nyerere kuwasaidia ili Yule mkoloni( sultan) asiweze kurudi Zanzibar ndio ikabidi kuungana na Tanganyika. Sultan alikuja na kuikuta Zanzibar na watu weusi wanaishi akajimilikisha. Ilikuepo ni muhimu apinduliwe aende akatawale huko kwao Oman .
 

Mkuu Sultan si mkoloni, Sultan alikua ni Mzanzibari, Nyerere hajawasaidia wazanzibar, na ndio mana Anachukiwa sana Zanzibar. Tatizo kubwa lililokuepo Bara wanaizungumza Zanzibar from their own point of view, Na sio kwa point of view ya Wazanzibari wenyewe.

Unachotakiwa kufahamu, Zanzibar ikiwa huru Kariokoo inazikwa kwenye masuala ya Biashara. kuwa na mwambao mkubwa kwa Bara haiwezi kuiathiri Zanzibar kwenye sera zake za biashara.
 
Sultan ni mkoloni wa Kwanza alieanzisha biashara ya utumwa Zanzibar. Kwani sultan alikuepo ni mtu mweusi au mtu mwenye asili ya Asia. Alipokuja mzungu alimtawala sultan na watu weusi Kwa pamoja. Sultan alitokea Oman . Sultan wa Oman wa sasa na Yule aliyepinduliwa Zanzibar ni mtu na mdogo wake. Asili Yao ni Oman Zanzibar walikuja tuu. Kwa taarifa yako Hadi maeneo ya mwambao wa kuanzia Mtwara mpaka Tanga ilikuepo ni miliki ya sultan. Hiyo yote iliitwa Zanzibar mzungu alikuja kupunguza mipaka ya Zanzibar je hii ilikuepo ni Mali yake au alijimilikisha tuu. Bila wapemba . Sasa kule Zanzibar wameondoka wamefuata circulation ya pesa inayopatikana Tanganyika. Kule Zanzibar hamna mizunguko wa pesa hata wakiondoka kule znz wataenda kufirisika kwasababu mizunguko upo Tanzania bara.
 

Kuwa asili ya familia yake ilitokea Oman hakumfanyi yeye kuwa ni mkoloni. Hivi Vice President wa sasa wa TZ nae ni mkoloni? Mana asili yake ni Burundi.

Tatizo kubwa linalowasumbua wabara ni kuiangalia Zanzibar kwa misingi ya kibaguzi. Acha Ubaguzi ndugu
 
kimbunga kinachokuja ni ushahidi tosha kwamba bara ni muhimu sana kwa zanzibar, kwasababu kwa dunia ya leo kuishi kisiwani ni risk sana (angalia ufilipino na japan), huku bara tunawapa ardhi, na visiwa vingi vinapotea over time kila mwaka vinapungua ukubwa kidogokidogo. wanzazibari msitukane mamba wakati hamjavuka mto.
 
KAbisa kabisa. NA imepigiwa mstari kabla hata ya kumsahau Nabii na Mfalme wetu. Hili halikubaliki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…