4% ya Watoto waliotumia Intaneti Tanzania walifanyiwa Ukatili wa Kingono

4% ya Watoto waliotumia Intaneti Tanzania walifanyiwa Ukatili wa Kingono

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ripoti ya Hali ya Ukatili wa Watoto Mtandaoni (Disruption Harm Report in Tanzania 2022/23) inaonesha 67% ya Watoto wenye Miaka 12-17 ni watumiaji wa Mitandao kupitia Simu na Kompyuta kutoka kwa Wazazi/Walezi.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii imeonesha kuna ongezeko la Watoto wanaoingia kwenye kundi la Wahanga wa aina mojawapo wa Ukatili Mtandaoni ikiwa ni pamoja na Kulazimishwa kujihusisha na Vitendo vya Ngono.

Matukio mengine ni pamoja na kurubuniwa Kusambaza Picha na Video zenye Maudhui ya Ngono bila Ridhaa yao na kujihusisha na shughuli za kingono kwa kuahidiwa Fedha au zawadi nyingine.
 
Back
Top Bottom