BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wizara ya Fedha na Mipango imesema asilimia 40 ya Watanzania bado hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Novemba 15, 2022 na Kamishna wa Uendelezaji Sekta ya fedha, Charles Mwamaja wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma kuhusu wiki ya fedha inayotarajia kufanyika kuanzia Novemba 21 hadi 26 jijini Mwanza.
Mwamaja amesema kazi kubwa inafanyika kupitia wizara hiyo ili wananchi waweze kuitambua sekta ya fedha na kufikiwa na huduma zake.
Amesema mbali na kutofikiwa kwa huduma ya fedha, lakini uelewa wa watu katika sekta hiyo bado upo chini ya asilimia 60 kwa sasa.
Amesema Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanakuwa na uelewa kuhusu sekta hiyo ifikapo 2025.
"Tutakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa makundi mbalimbali na wadau wa Fedha, tunaamini uelewa wa masuala ya fedha utaongezeka ili kupunguza kundi hili la asilimia 40 ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha," amesema Mwamaja.
Kuhusu wiki ya fedha amesema watatumia muda huo kuendesha madarasa maalumu ambapo taasisi na wadau wa huduma za kifedha wamealikwa kushiriki.
Kauli mbiu ya wiki hiyo inayofanyika viwanja vya Mwanza City ni Elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya Watu ambapo amefungua milango kwa mikoa jirani kushiriki maonyesho hayo.