4G ya Halotel ni utapeli

4G ya Halotel ni utapeli

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Halotel hawana 4G

Narudia hawana 4G

Ninaishi katikati ya mji kabisa mita kadhaa tu kutoka minara yao ilipo lakini cha ajabu speed yake ni ya kobe yaani hata kb haifiki inatembea 5 bps yaan byte yaani hata kb hawafiki.

Ukiona imesoma hata 2.2k/s hapo ndo imejitahidi.

Nilidhani ni nyumbani nimezunguka maeneo mengi ya Dar kwenye hekaheka zangu speed ni hiyo hiyo tu ya kobe yaani wakijitahidi sana ni 20kb per second.

Hawa nao wana 4g? 4g ya nchi gani hii?halotel ni matapeli wa karne hawakuzindua 4g waliudanganya umma kwa maksudi

Ukweli halotel hawana 4g wala nini ni uwongo na utapeli.

Pia niwaambie namalizia research yangu fulani hivi kuhusu networks hapa tz nisiongee sana kuna mazito aisee kuhusu hii mitandao na ukweli nitaumwaga hapa.

Halotel acheni utapeli hamna cha 4g wala nini oneni mtandao wa hovyo duuuh[emoji1313][emoji1313]

Screenshot_20210721-223650.jpg
 
hata Vodacom kuna baadhi ya maeneo hapa nchini wanatu piga…..
 
Unamalizia research yako afu tayari ushakuja na conclusion...

Itabidi upewe kitengo tcra
 
Huenda kwako tu
Mm mbona inagonga hadi mb 8 kwa sekunde na ndio nipo huku kijijin kabisa yaani inakimbiza kuliko hata Tigo na Voda

Kiufup hakuna mtandao ulio slow au fasta ila inategemeana na eneo ulipo
 
Mb 8 per second huo ni udhaifu mkubwa mkuu...kumbuka 4g inatakiwa iende hadi 300 mb per second
 
Mb 8 per second huo ni udhaifu mkubwa mkuu...kumbuka 4g inatakiwa iende hadi 300 mb per second
Naiona bora hata hyo 8mb ya halotel Tigo ikizidi sana ni 3mb per second Voda ndio kabisaaa hata 4G hawana ni 3G na hapo spid ikizid sana ni 600kb per second
 
Naiona bora hata hyo 8mb ya halotel Tigo ikizidi sana ni 3mb per second Voda ndio kabisaaa hata 4G hawana ni 3G na hapo spid ikizid sana ni 600kb per second
Voda kwangu inatembea 50 mbps
 
tumekusikia, ila mitandao ipo mingi si lazima ukomae huko ulipo!!
 
Nimejaribu kuangalia hiki unachosema kwa kusajili line ya halotel 4G mbona iko vizuri sana? Kwangu inasoma mpaka 23.6Mb/s
 
Back
Top Bottom