4WD ya IST na Kluger, je ni full time ama on-demand?

Kaveli

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
5,443
Reaction score
8,903
Hello wajuvi wa gereji ya Jf,

Kama Subject title inavyojieleza, kuna jamaa yangu angependa kufahamu... IST and/or Kluger, 4WD yake ni FULL TIME? ama ni ON-DEMAND (kuiweka anapotaka dereva)?

Thanks comrades.

-Kaveli-
 
Kwa uelewa wangu, gari ndogo za Toyota (Kluger, Rav4, sina uhakika na IST) nyingi hazina Four Wheel Drive (4WD), zina kitu wanaita All Wheel Drive (AWD). Tofuati kubwa kati ya 4WD na 4WD inakuwa engaged na dereva, wakati AWD inawekwa na ECU ya gari.

Sasa kwa mfumo wa Toyota kwa gari ndogo, AWD ni on demand, sio full time. Hizo gari zote ulizotaja hapo ni basically front wheel drive, lakini kama ina option ya AWD, huwa inaingia pale tu ECU inaposense kuwa kuna tairi moja au yote ya mbele yanateleza au yamepoteza traction, hapo ndio diff ya nyuma inapewa taarifa kuengage ili tairi za nyuma zizunguke.

Subaru wao AWD ni full time. Japo pia nguvu inagawanywa tofauti kwa tairi za mbele na za nyuma wakati gari linatembea kwenye barabara nzuri mbele nguvu inakuwa 60% nyuma 40% ili kuokoa mafuta.
 
👏👏👏👏👏
 
Wewe ni fundi!Jibu murua kabisa Mkuu
 
Mkuu samahani bado sijakuelewa vizuri apo kwenye utofauti kati ya 4WD na AWD...4WD ni Four Wheel Drv na AWD ni All Wheel Drive sasa kwani Gari si lina Matairi Manne?....bado napata mkanganyiko wa 4WD na AWD ukizingatia Tairi zipo nne kwenye Gari
 
Kuna 2WD na 4WD...

2WD ni tairi 2 tu za mbele ndizo zinavuta gari.. 4WD ni tairi zote zinafanya kazi.

Kama ulishawahi kumiliki au kuendesha gari kabla ya haya automatic kujaa utakuwa unalijua hili.. Kama ulishawahi kupanda manual car utaona kuna gear river 2, kubwa na ndogo, ile ndogo ndiyo hutumika kuengage 4WD hasahasa ukiwa unapita kwenye rough road kama kwenye tope au mlima mkali..
 
HIVI KATI YA GARI INAYOVUTA MBELE" FRONT WHEEL DRIVE", NA INAYOVUTA/KUSUKUMA NYUMA" REAR WHEEL DRIVE" IPI INAFAA KATIKA MATUMIZI YETU DAILY. HUSUSANI KATIKA ROADS ZETU
 
HIVI KATI YA GARI INAYOVUTA MBELE" FRONT WHEEL DRIVE", NA INAYOVUTA/KUSUKUMA NYUMA" REAR WHEEL DRIVE" IPI INAFAA KATIKA MATUMIZI YETU DAILY. HUSUSANI KATIKA ROADS ZETU
Kwa mambio+Stability nina prefer RWD lakini shida ya hizi RWD ni kukwama kwny matope/utelezi hata kidogo tu umeshanasa tayari.

FWD hua iko poa sana hata kwny matope unaweza kujinasua 'kirahisi' kiasi compared to RWD.
 
Mkuu samahani bado sijakuelewa vizuri apo kwenye utofauti kati ya 4WD na AWD...4WD ni Four Wheel Drv na AWD ni All Wheel Drive sasa kwani Gari si lina Matairi Manne?....bado napata mkanganyiko wa 4WD na AWD ukizingatia Tairi zipo nne kwenye Gari
ngoja nimsaidie mdau hapo juu

kwenye kila nyanja kuna lugha zake..

sasa ukija kwenye magari upande wa drivetrain kuna lugha zifuatazo...

2WD -Front wheel drive/ Rear wheel drive....

AWD- tairi zote nne zinazunguka either full time au kwa ECU kujiseti yenyewe pale penye uhitaji dereva huna mamlaka nayo yenyewe ipo inajipeleka yenyewe... na mgawanyo wa power kwenyw matairi huwa sawa 50/50 au 40/60

4WD (4×4) gari inakuwaga moslty ni REAR WHEEL DRIVE na ukitaka yazunguke yote manne basi dereva itabidi utoe comand by a touch of a button au kwa kutumia gear ya 4X4 mgawanyo power huwa haupo sawa mara zote tairi za nyuma huchukua 80 na za mbele hupata 20.. na siyo recomended for a long run na wala speed hutakiwi kuvuka 60

nahisi ntakuwa nimesaidia kidogo

so hadi hapi utakuwa umeona tofauti ya AWD na 4WD

AWD ipo automatic full time na mgawanyo wa power upo 50/50 au 40/60

4WD hii dereva unaweka mwenyewe kuruhusu matairi ya mbele yavute kutokana na mazingira uliyopo na huruhisiwi kuitumia muda wote utaharibu gari...mara tu unapotoka kwenye eneo tata unatakiwa ui dis-engage
 
La tano liko nyuma
Mkuu samahani bado sijakuelewa vizuri apo kwenye utofauti kati ya 4WD na AWD...4WD ni Four Wheel Drv na AWD ni All Wheel Drive sasa kwani Gari si lina Matairi Manne?....bado napata mkanganyiko wa 4WD na AWD ukizingatia Tairi zipo nne kwenye Gari
 
Mkuu samahani bado sijakuelewa vizuri apo kwenye utofauti kati ya 4WD na AWD...4WD ni Four Wheel Drv na AWD ni All Wheel Drive sasa kwani Gari si lina Matairi Manne?....bado napata mkanganyiko wa 4WD na AWD ukizingatia Tairi zipo nne kwenye Gari
Gari yenye 4WD, kwa kawaida nguvu iko kwenye matairi mawili, hasa ya nyuma. Hiyo 4WD ni dereva ndio anaamua kuiwasha pale kunapokuwa na uhitaji. Na hapo matairi yote manne yanatembea kwa nguvu sawa. Kama kwenye Land Cruisers na magari makubwa kama hayo. Japo na madogo yapo pia. AWD kwa system ya Toyota na kampuni nyingine nyingi, tairi mbili, hasa za mbele ndio zinafanya kazi muda mwingi, ila computer ya gari inauwezo wa kuzungusha matairi yote manne kwa wakati wake bila dereva kufanya lolote, hasa pale computer inapogundua tairi moja au mawili yanazunguka bila kulisukuma gari. Yaani yanaslip kama kwenye tope. Sasa hii ndio ina full time na on demand.

So kwa kifupi, hayo majina 4WD na AWD yametumika ili kutusaidia kuelewa tofauti kati ya hiyo mifumu miwili inayokaribiana saana.
 
Nice one
 
Kwa mambio+Stability nina prefer RWD lakini shida ya hizi RWD ni kukwama kwny matope/utelezi hata kidogo tu umeshanasa tayari.

FWD hua iko poa sana hata kwny matope unaweza kujinasua 'kirahisi' kiasi compared to RWD.
RWD handling yake safi saana. As tairi za mbele kazi yake ni kuongoza gari tu kwenye uelekeo sahihi
 
Shukrani kwa maelezo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…