50+ angalieni afya zenu kujiepusha na magonjwa sugu na vifo vya ghafla

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ukifisha miaka 50+ metabolism inabadilika kutokana na aging process. Ni muhimu kubadilisha life style, kama ni mnywaji punguza kiwango cha pombe, ongeza kiwango cha mboga na matunda katika mlo na pia kufanya mazioezi hata kutembea kwa saa moja kila siku kunasaidia.

Magonjwa kama kisukari
Hypertension yasipoangaliwa husababisha stroke.

Kupima PB na sugar levels kwenye damu kunaokoa maisha na pesa nyingi za gharama za matibabu.
 
Ubarikiwe
 
Sahihi kabisa. Hata walio chini ya miaka 50 wanahitaji kuzingatia misingi ya lishe, kufanya mazoezi, kupunguza matumizi ya vileo na kupima afya zao mara kwa mara.
 
Dunia haina haki, fikiria ulipokuwa shule ulikula ugali maharage, chuo ulikula bilinganya na wali. Ulipoanza kazi ulikula sana mchicha ukijipanga. Sasa uko 50 na kiposition kazini unaambiwa upunguze kula nyama na bia.
 
Aiseee kuna siku nilikwenda kumtembelea bro sasa wakati tunatoka nikaona pipe juu nikapiga push-up kama 15. Kushuka nikamwambia bro jaribu utapiga ngapi alijaribu nasikia kelele na pumzi kibao zikimtoka. Nikamwambia unahitaji mazowezi bro manake kwenye kula huyu bro anakula hatareee. Mazoezi na afya bora, ndio msingi mzuri wa maisha

Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Kama ni mzito sana aanze kupungua kwa diet kwanza ndiyo aanze push ups. Anaweza kuanza kutembea au jogging mdogo mdogo
 
Dalili nzuri ni kuwa na flat tummy, kitambi si dalili nzuri
Nilianza kupiga push-up darasa la saba hadi sasa, kifua kimevimba kama baunsa hadi najichukia, ila siwezi acha
 
Dunia haina haki, fikiria ulipokuwa shule ulikula ugali maharage, chuo ulikula bilinganya na wali. Ulipoanza kazi ulikula sana mchicha ukijipanga. Sasa uko 50 na kiposition kazini unaambiwa upunguze kula nyama na bia.
Halali imegeuka haram
 
Mazoezi yaliyo bora ni kukimbia. Jogging yaani kila sehemu ya mwili inakua activated.
 
Dunia haina haki, fikiria ulipokuwa shule ulikula ugali maharage, chuo ulikula bilinganya na wali. Ulipoanza kazi ulikula sana mchicha ukijipanga. Sasa uko 50 na kiposition kazini unaambiwa upunguze kula nyama na bia.
World not fair bora ellian wawo hawapitii changamoto kama hizi kwenye sayari yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…