Uchaguzi 2020 55 wajitokeza kuutaka Ubunge wa Chato kupitia CCM

Uchaguzi 2020 55 wajitokeza kuutaka Ubunge wa Chato kupitia CCM

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Katika hali iliyowashangaza wengi, watia nia wapatao 55 wamejitokeza kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, ili wapitishwe kugombea Ubunge Jimbo la Chato.

Ikumbukwe kwamba Jimbo la Chato ndiko nyumbani kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli ambaye aliliongoza jimbo hilo kwa miaka 20 mfululizo kwa mafanikio makubwa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.

Katika vipindi vinne alivyoliongoza jimbo hilo ambalo zamani liliitwa Biharamulo Mashariki, Rais Magufuli alipita bila kupingwa katika vipindi viwili.

Miongoni mwa waliochukua fomu mwaka huu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani anayetetea nafasi yake.

Taarifa kutoka Chato zinadai Dkt. Medard Kalemani anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vijana wasomi wazawa wa Chato ambao wamejitokeza kumpinga.

Uwepo wa watia nia 55 wengine wameutafsiri kuwa ni kutokana na mwamko mkubwa na demokrasia iliyokomaa ndani ya CCM ambapo sasa wanachama wote wana nafasi sawa ya kugombea tofauti na zamani ambapo walio na fedha ndio walikuwa na nafasi.

Pia inadhihirisha kauli ya Rais Magufuli kwamba hana mgombea na kwamba hajatuma mtu kwenda popote kugombea bali kura za wajumbe ndizo zitakazoamua.
 
Demokrasia: 55 wajitokeza Ubunge Jimboni kwa Rais Magufuli

Katika hali iliyowashangaza wengi, watia nia wapatao 55 wamejitokeza kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, ili wapitishwe kugombea Ubunge Jimbo la Chato.

Ikumbukwe kwamba Jimbo la Chato ndiko nyumbani kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli ambaye aliliongoza jimbo hilo kwa miaka 20 mfululizo kwa mafanikio makubwa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.

Katika vipindi vinne alivyoliongoza jimbo hilo ambalo zamani liliitwa Biharamulo Mashariki, Rais Magufuli alipita bila kupingwa katika vipindi viwili.

Miongoni mwa waliochukua fomu mwaka huu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani anayetetea nafasi yake.

Taarifa kutoka Chato zinadai Dr Medard Kalemani anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vijana wasomi wazawa wa Chato ambao wamejitokeza kumpinga na wakionekana kuwa na ari ya kuleta mabadiliko zaidi.

Uwepo wa watia nia 55 inaonyesha mwamko mkubwa na demokrasia iliyokomaa ndani ya CCM ambapo sasa wanachama wote wana nafasi sawa ya kugombea tofauti na zamani ambapo walio na fedha ndio walikuwa na nafasi.

Pia inadhihirisha kauli ya Rais JPM kwamba hana mgombea na kwamba hajatuma mtu kwenda popote kugombea bali kura za wajumbe ndizo zitakazoamua.

Mbali na Kalemani mtia nia mwingine anayeonekana kuwa na ushawishi kwa wana Chato ni Mhandisi Andrea Kasamwa.

Idadi hii ya watia nia inaonesha dhahiri kuwa demokrasia si tu ndani ya CCM imezidi kuimarika lakini ni kiashiri cha dhamira ya Serikali ya Magufuli kuwapa watanzania fursa pana ya kushiriki siasa.
 
Demokrsia ya fom moja ya mgombea wa uraisi ama kweli ukiwa uwongo ndio msingi wa kukubalika
 
Kwa kwenzi zile ngoja wasubiri baadaye huenda hali ikatulia
 
Sawa tunaunga Juhudi za raisi Jpm.

Pamoja na uhaba wa ajira na masilahi ya kazi zao
 
Sema Ngosha enzi zake alikuwa anapita kibabe sana huko.
 
Hivi kuna jimbo lolote ambalo wamejitokeza wagombea hata 20 kupitia vyama vya upinzani kwa ujumla wao?
 
Hivi kuna jimbo lolote ambalo wamejitokeza wagombea hata 20 kupitia vyama vya upinzani kwa ujumla wao?
Subirin chadema iwafokonyoe vizur unafikir kuhamasishana kwenu ili kuwaaminisha watu kuwa ccm inakubalika ndo mtashinda tulieni nyinyi.
 
Back
Top Bottom