Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
Apple imeongeza 5G support katika maeneo mbalimbali duniani. Tanzania ni moja kati ya maeneo ambayo sasa watumiaji wa iPhone 12 na kuendelea wanaweza kupata mtandao wa 5G.
Kwa ripoti nyingi zinaonyesha baadhi ya maeneo ambayo kwa iOS 16.4 yamepata support ya 5G ni Macau na Uturuki. Lakini kwa Tanzania pia nimeona tayari settings za 5G zimeanza kupatikana na kama unatumia mtandao wa Vodacom au tiGO utaona settings hizo zinapatikana na ukiwasha indicator inaonekana.
Inawezekana pia kwa watumiaji wa Kenya, na nchi nyingine za Afrika Mashariki wanaweza kupata sehemu hii.