5m kwa ujenzi Mbeya

5m kwa ujenzi Mbeya

Waambi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
737
Reaction score
81
Najua si rahisi Dar kujenga nyumba kwa mil.5. Naomba kujua kama hela naweza kujenga nyumba ya kawaida Mbeya, Matofali ya kuchoma.
 
Inatosha kwa sababu hapohapo kiwanjani utachimba udongo wa kufyatua matofali.
 
Toa kwanza tafsiri ya "nyumba ya kawaida" ili tujue itatosha au vipi.
 
Nyumba yenye vyumba.5 vyenye ukubwa wa wastani
 
Nyumba yenye vyumba.5 vyenye ukubwa wa wastani

M5 ni nyingi kwa ujenzi mkuu, ila sitaki nikupe matumaini ya kukamilisha nyumba ya vyumba vitano kwa hiyo pesa.
Achilia matofali, kuna suala la lenta, mabati, mbao za kuezekea na mbaya zaidi finishing,hiyo finishing ndio inaweza kukatisha tamaa kabisaa.

Ila kama una hiyo pesa, na una uhakika wa kupata nyingine baadae, anza ujenzi. Kama hauna uhakika wakupata nyingine tafakari upya namna ya kuiongezea hiyo pesa, vinginevyo utafika mahali umeshaanza kujenga na huwezi kuimalizia nyumba yako mkuu.

"Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza"

Luka 14:28-30
 
Samaritan asante kwa ushauri wa busara. Ila kiwanja kipo tayari
 
nitafutie nami kiwanja huko mbeya best naitaji sana nami nianze ujenzi huko
 
Samaritan asante kwa ushauri wa busara. Ila kiwanja kipo tayari

Karibu mkuu, unajua naongea kitu ambacho nna kifaham. Na hapo bado palikuwa panatakiwa tiles, rangi ndani na nje, vifaa vya umeme, vioo vya madirisha, vifaa vya vyooni/bafuni. Ila unaweza ukaamua kuvifanya kwa awamu na kuna baadhi ya vitu unavimalizia ukiwa ndani tayari. Hii ni huko kijijini.
. View attachment 119667

2013-03-23 18.10.40.jpg

View attachment 119669
 
huwezi!

kwa maeneo yaliopimwa huwez fyatua tofali hapo hapo so itakubidi ununue!gharama za fundi si pungufu ya 1.5,cement 18,000/= kwa mfuko,hujafika kwenye renter na bei ya nondo inapanda kila asubuhi,itakusogeza sogeza ila kujenga kabisa ngumu bosi!
 
Kawaida vyumba viwili vya kulala, sebule, jiko, etc au ? kawaida kwako kwa MWENZIO ni mansion etc
 
Najua si rahisi Dar kujenga nyumba kwa mil.5. Naomba kujua kama hela naweza kujenga nyumba ya kawaida Mbeya. Matofali ya kuchoma
Mkuu kwani ujenzi wa nyumba ni tofali tu? ila kama unataka kujenga nyumba iliyokamilika kwa maana finishing ni vyema ukatambua vifaa vingi vya finishing ni ghalama huko mikoani kwani asilimia kubwa vinatokea dar so ghalama za usafirishaji hufanya vikifika huko ghalama kuwa kubwa kuliko dar. Nahisi kwa nyumba unayifikiria wewe huko mbeya ni rahisi kuijenga ukiwa dar pia.
 
Back
Top Bottom