6 million Kenyans are facing hunger

Ready to feed hunger stricken Kunyans
 
Aendelee kuwafungia tu wenzao zambia nakonde walitoleana uvivu ni hivii nchi kubwa zenye uwezo na nyenzo na sayansi ya hali ya juu zimenyoosha mikono kwa covid sembuse nchi zinazo jikongoja kwa kunyonywa na haohao walio leta covid, mtaiweza!!!? Misaada itoke hukohuko tena kwa riba! Fungulieni watu watafia ndani
 
Jamani nchi yenye uchumi wa kati ina njaa!! MK254 hapa hatokei. Unatakiwa msaada wa haraka!!
 
Mbona MK254 hatokei hapa atueleze vizuri hali ya nchi yake yenye uchumi wa kati? How can the two be reconciled? ie njaa always na uchumi wa kati?? Nini faida ya uchumi wa kati kwa hawa wanaolia njaa kila mwaka? Hapo ndio mjue kuwa criteria inayotumika ya GDP ni kiini macho mtupu!! Kama Tsifa inaonekana mnazalisha sana lakini kumbe kinachozalishwa kinamilikiwa na mabepari (weupe na weusi) wachache! Mliobaki wenzangu na mimi kina MK254 mnaambulia kuimba tu pambio za "Taifa la uchumi wa kati" wakati huo uchumi unausikia tu kwenye bomba!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania yaongoza kuuza mahindi Kenya
habarileo.co.tz


MVUA kubwa zilizonyesha kuanzia Oktoba mwaka jana hadi Mei, mwaka huu zimesababisha mahindi mengi yanayotarajiwa kuvunwa nchini Kenya kuwa katika hatari ya kuwa na sumukuvu inayotokana na kuvunda baada ya kuingia maji yakiwa yamekomaa.

Hali hiyo pamoja na uvamizi wa nzige wa jangwani walioingia katika kanda zenye wakulima wengi wa mahindi yakiwemo maeneo ya Turkana na Pokot na kuharibu mazao, kumesababisha uhaba mkubwa wa chakula nchini Kenya pamoja na kupanda kwa bei ya mahindi sokoni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Kenya, Hamadi Boga, aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi juzi kuwa, katika kipindi cha kuanzia jana hadi Julai 30, mwaka huu, wanategemea mahindi kutoka Tanzania kwa sababu wakulima wa nchi hiyo wanasubiri kuvuna mahindi yao mwezi Agosti hadi Septemba, mwaka huu.

Alisema Tanzania ndio muuzaji mkubwa wa mahindi nchini Kenya na katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Kenya ilipokea mahindi kiasi cha magunia milioni mbili kutoka nchini, kati ya magunia milioni 4.2 ya mahindi meupe yanayohitajika kila mwezi kwa ajili ya chakula cha wananchi.

“Wafanyabiashara wameingiza mahindi katika soko la Kenya kutoka nchi jirani kwa sababu katika kipindi cha kuanzia Juni hadi Julai 31 tutakuwa hatujaanza kuvuna mahindi labda kuanzia Agosti au Septemba mambo yatatengamaa sokoni,” alisema.

Boga alisema mbali na magunia milioni mbili ya mahindi meupe, serikali ya Kenya pia iliagiza mahindi ya njano kutoka nchini Mexico kiasi cha magunia milioni mbili kwa ajili ya chakula cha wanyama.

Alisema kuruhusu mahindi kuendelea kuingia nchini Kenya kutoka nchi jirani kutasaidia kupunguza uhaba mkubwa wa mahindi na pia kutasaidia kushusha bei ya bidhaa hiyo pamoja na unga wa mahindi katika soko.

Boga alisema taifa lake linapitia katika kipindi cha mpito kutokana na changamoto ya mvua kubwa zilizonyesha mwezi uliopita, kipindi ambacho ni muhimu kwa mahindi kukomaa na kukauka.

Kutokana na mvua hizo, Wizara ya Kilimo inaamini kuwa wafanyabiashara wengi wa Kenya watayakataa mahindi kutoka kwa wakulima wa nchi hiyo na kuendelea kuagiza mahindi kutoka Tanzania kwa sababu ya ubora na bei nafuu.

Baadhi ya wafanyabiashara wamelalamikia hatua ya serikali kuagiza mahindi kutoka Mexico, wakisema mara nyingi yanakuwa hayana viwango vilivyokubalika katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Mahindi kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanakuwa yamepitia katika viwango vya ubora vilivyokubaliwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini hayo mahindi ya njano kutoka nje ya EAC yanakuwa hayana viwango hivyo,” alisema Okiya Omtatah, ambaye ni mwahaharakati na mtetezi wa walaji wa bidhaa nchini Kenya.

Mkurugenzi Mkuu wa wafanyabiashara wa mahindi nchini, Kenya Paloma Fernandes, alisema mbali na shehena ya mahindi kutoka Tanzania ambayo tayari yapo sokoni, wanatarajia kuwa shehena nyingine itaingia nchini humo katikati ya mwezi huu.

Wiki iliyopita Waziri wa Kilimo nchini, Japhet Hasunga, aliliambia Habarileo Afrika Mashariki kuwa, kutokana na serikali kuwajali wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwa bei nafuu, kumewawezesha wakulima wengi kuzalisha mazao mengi yenye viwango vya kimataifa.

Alisema viwango hivyo vimekuwa vikiyawezesha mazao kutoka Tanzania kukubalika katika masoko yote katika nchi za Afrika Mashariki zikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kisdemokrasia ya Kongo (DRC).

Alisema pamoja na changamoto ya mafuriko sehemu mbalimbali na janga la virusi vya corona, wakulima wa Tanzania waliendelea kufanya kazi kwa bidii na ana amini mavuno ya mwaka huu yatakuwa mengi kiasi cha kuifanya serikali kuwa na chakula cha kutosha huku cha ziada kikiendelea kuuzwa nje ya nchi kupitia kwa wakulima.

Tanzania yaongoza kuuza mahindi Kenya
 
Hawa jamaa wanajifanya wana undugu na wazungu, wakaombe msaada huko
 
Poleni sana majirani, nina akiba ya animal feed leteni hela niwauzie inaweza saidia kuondoa njaa
 
WFP wapigaji tu, anyway, walete hizo pesa tuwauzie unga, sio mahindi, tutawauzia unga..! Hawataki wachukue time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…