Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Asilimia 72 ya fedha za ruzuku inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwapatia pesa ya motisha walimu, hazifiki shuleni na kuwafanya walimu hao kukosa ari ya kufundisha.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji ya Sekta ya Elimu ya mwaka 2010 hadi 2011, ruzuku hiyo ilikuwa haifiki kama iliyopangwa na ilikuwa ikipungua katika miaka ya hivi karibuni. Asilimia 28 tu ya ruzuku ndiyo inayofika shuleni na wala si kwa wakati unaotakiwa.
Meneja wa mawasiliano wa shirika lisilo la kiserikali la Twaweza, Risha Chande, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa baada ya kuona tatizo hilo Twaweza imeamua kuanzisha mpango wa Kiu ya ujifunza (KiuFunza) utakaojihusisha na kupeleka kiasi kamili cha ruzuku ya uendeshaji kwa walengwa kwa wakati ili kuboresha elimu nchini.
Chande alisema kuwa mpango huo umezinduliwa kwa lengo la kupeleka fedha za kuwalipa walimu motisha.
Alisema Mpango huo utatekelezwa katika Halmashauri 11 zilizochaguliwa na katika kila wilaya shule 35 zitashiriki. Wilaya zitakazohusika katika mpango huo utakaotekelezwa katika kipindi cha 2013 na 2014 ni Karagwe, Kigoma Vijijini, Geita, Kahama, Kondoa, Korogwe Vijijini, Lushoto, Sumbawanga Vijijini, Mbozi, Mbinga na Kinondoni.
Mkuu wa Twaweza, Rakesh Rajani, alibainisha kuwa Tanzania inaelekea kufikia lengo la elimu kwa wote na sasa upo uwiano sawa kati ya watoto wa kike na wa kiume katika shule za msingi, lakini changamoto iliyopo ni kuinua ubora wa kujifunza.
SOURCE: NIPASHE