7UP : ASILI YA JINA LA SODA YA 7up

7UP : ASILI YA JINA LA SODA YA 7up

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Mwanzoni wakati kampuni inaanzishwa kilitengenezwa kinywaji cha limao(lemon) mmiliki Charles Leiper Grigg akatoa kazi kuwa anatafuta jina la kipekee na linalo vutia macho ya watu kwaajili ya kinywaji hicho kipya cha limao(lemon).

Wabunifu walitengeneza majina mengi, ila katika majina yote ni jina moja tu lilikua la kipekee na linalovutia macho ya watu, jina lenyewe ilikua ni 7up lilivutia macho ya watu hata kabla ya kujulikana maana yake ni nini.

Kwakua wabunifu wa majina hayo walikua wamekusanyika pamoja tajiri Grigg akauliza hili jina 7up linamaana gani? Lakini cha ajabu ni kuwa hakuna aliejibu, ikabidi Grigg asome jina la mtu aliebuni jina hilo la 7up.

Aliposoma jina la mbunifu aliependekeza hilo jina, Grigg akamuuliza yule mbunifu kwanini nimekuomba unifafanulie jina hili 7up lina maana gani ila ulikaa kimya? Yule mbunifu wa jina akajibu kwa kusema mimi sijapendekeza hilo jina, ila nilipendekeza herufi tatu tu ambazo ni dnL ambayo ni kifupi cha (drink national Lemon) ila wewe uliigeuza juu chini badala ya kusomeka dnL ukasoma 7up, licha ya ufafanuzi huo ila ikaonekana hivyo hivyo lilivyogeuzwa ndo linavutia, na rasmi kinywaji hicho cha limao(lemon) kikapewa jina la 7up.

Kwahiyo muda mwingine mambo huenda kinyume na tulivyopanga lakini kwenda kwake kinyume ndo bor
FB_IMG_1739538838193.jpg
a zaidi.
 
Kwenye brands kunakuwa na stories nyingi saana hasa ndugu zetu motivational speakers..
Wengine wanasema limetokana na 7 ingredients...tushike lipi?
Hapa hakuna lakushika utashikwa wewe ukizubaa chakufanya fungua kizibo ibariki nafsi wenye kuleta stori walete tu huku tunaduguda!
 
Red Bull kipindi wanaanzisha kampuni walitumia mbinu ya kutupa makopo tupu ya Red Bull mitaani, hasa kwenye sehemu za burudani , stand za magari na treni na vilabu vya usiku, ili kuunda hisia kwamba kinywaji hicho kilikuwa maarufu sana na kinanyweka kwa wingi.

Mbinu hii ilipelekea watu wazidi kununua zaidi kinywaji hiko wakifikiria kuna kitu cha ziada kwa sababu ilionekana kinanyweka zaidi.
 
Basi nikajua bosi alivyoona majina yote mabaya ikabidi aanze kuwaadhibu aliowapa kazi ya utunzi wa jina ile anafika yule wa saba sasa mtunz mwenyewe alikuwa haelew ikabidi bosi atie Mkazo kidogo SEVEN UP wa saba amka sasa katika kulopoka kwa saut ndio mmiliki wa kiwanda akasikia jina zuri limetamkwa 7up
 
Red Bull kipindi wanaanzisha kampuni walitumia mbinu ya kutupa makopo tupu ya Red Bull mitaani, hasa kwenye sehemu za burudani , stand za magari na treni na vilabu vya usiku, ili kuunda hisia kwamba kinywaji hicho kilikuwa maarufu sana na kinanyweka kwa wingi.

Mbinu hii ilipelekea watu wazidi kununua zaidi kinywaji hiko wakifikiria kuna kitu cha ziada kwa sababu ilionekana kinanyweka zaidi.
Jamaa katupiga kamba

7up maana yake ni kuwa imara siku Saba za week
 
Waliiga Sprite kutoka kampuni ya Cocacola. Jinsi Pepsi ilivyoiga Cocacola . Mirinda orange kuiga Fanta orange (soda za madenti na madem)
 
Wamezunguka tu ila idea ya hicho kinywaji imetokana na Sprite
 
Back
Top Bottom