80% ya wabunge/madiwani/rais/mawaziri wamedumaa akili

80% ya wabunge/madiwani/rais/mawaziri wamedumaa akili

Kokolo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2008
Posts
1,985
Reaction score
3,310
Hali ya Taifa hili ni mbaya sana. Na tusipoangalia, Taifa hili tutalipeleka shimoni kabisa. Tangu mwaka 2007, Asilimia 38% ya watanzania wamedumaa akili kutokana na lishe duni. Maana yake nini? Maana yake katika kila watanzania 100, watanzania 38 wamedumaa akili, hawafikiri vizuri kutokana na lishe duni.

Lishe duni ni ‘indicator' ya ufukara.

Kama madiwani wa CCM ni watanzania wa kawaida, basi katika kila madiwani 10, madiwani 4 wamedumaa akili. Au katika kila wabunge 10 (wa CCM lakini), wabunge 4 wamedumaa akili kama wanatoka familia za kawaida. Hivyo hivyo kwa mawaziri wa serikali ya CCM, kwamba inawezekana katika kila mawaziri 10, mawaziri 4 wamedumaa akili. Pengine ndio sababu wamekuwa wanasaini mikataba mibovu ya kifisadi.
 
Inawezekana! maana mambo yanayofanyika nchi hii hayafai ata kuyaelezea
 
Mhhh!! ni ukosefu wa 'chakula' tu Mkuu au kuna lingine?? manaake muonekano wao na jinsi walivyo nyambuka..sidhani kama ni ukosefu wa chakula....labda lishe bora.
 
Hongera nayo hii ni mojawapo ya njia za kunyambulisha ufisadi.
 
Nafikiri research hii ilifanywa na Wazungu....Na sisi kazi yetu ni kuamini tuuu basi sababu zimesemwa na wazungu. teh teh teh
 
Nafikiri research hii ilifanywa na Wazungu....Na sisi kazi yetu ni kuamini tuuu basi sababu zimesemwa na wazungu. teh teh teh


Hivi nyie mlisha fika, namtumbo, nanyambe, rubale, nafuba, kamasi, Yaani nina maana maisha ya vijijini haswa!.

Huwezi shangaa matokeo ya tafiti hii kama ulisha wahi fika huko. Nyie kijijini maisha magumu asikudanganye mtu bwana!
 
Last edited:
KOKOLO,
Hizi data umezipata katika utafiti gani?

Wala huhitaji kuzipata kutoka kwenye utafiti. Wewe angalia tu jinsi Watanzania na Waafrika wengi wanavyoishi na mazingira waishiyo. Kamwe, narudia tena, kamwe watu wenye akili hawawezi kuishi maisha ya namna hiyo.

Watu wenye akili watatumia akili yao kuyamudu mazingira yao ili kuboresha maisha yao.
 
80 = 38 ??? Hautakiwi kutupa source umeeleweka
 
Hii himo kwenye ripoti ya umasikini ya serikali ya mwaka 2007, ila mwandishi ameongezea kwani ni 38%. Ni kweli ukosefu wa chakula bora bora unsababisha kudumaa kwa akili ndio maana hata shule zinazotoa lunch kwa wanafunzi wake mchana zinafanya vizuri kuliko ambazo hazitoi lunch.

Vilevile hii unaweza kuiona katika mazingira ya kila siku kwani ni kweli kabisa watanzania hatuwezi kuadapt mazingira na kuyatumia kwa manufaa yetu bali kila kitu tunasubiri kufanyiwa na serikali.

Inawezekana utafiti ulipunguza hii rate maana umefanywa na serikali kupitia kwenye mkukuta, ripoti hipo kwenye website ya mkukuta, kwa hapa naweza kumwelewa mwandishi kuwa aliongeza kwa kuona inawezekana mkukuta walipunguza kwa kuiokoa serikali kama Mwakyembe alivyofanya kwenye RD
 
Du hii inatisha!

Ni kweli kabisa ukiangalia umri wa wabunge wengi ni kuanzia 40 t0 80s.

na wale waliopo 40 to 50 ni wachache, wengi wao ni 50 to 80. Sasa hao ndio tunawategemea watunge sheria, wajadili budget, wapitie au wahoji mikatabu. Kwanza kuyasoma makabrasha tu ni wavivu.

Umri wa ubunge inatakiwa uwe kuanzia 35 to 55.

Mtu akishafikia umri wa kustaafu hastahili kugombea ubunge. Bungeni sio mahali pa kupumzikia.

Akistaafu hata kama ni maarufu arudi kijijini kwake na mafao yake akafungue miradi yake ya kilimo na ufugaji au akafanye shughuli za kijamii.

Hii inapaswa kupiganiwa na wanaharakati ili bunge lipitishe kuwa sheria.
 
Hizi data umezipata katika utafiti gani?


Jinsi tunavyoongea, jinsi tunavyoendesha magari ( kutanua na kuchomeka) jinsi tusivyofuata utaratibu ( passing the traffic lights, no quing etc, jinsi tuvyotupa taka na chupa za maji kila sehemu, jinsi tusivyofanya kazi (kwa wasio na kazi ), jinsi tunavyoshindwa kufanya kazi ipasavyo ( kwa wenye kazi).
 
yaweza kuwa kweli ila swali ni kwamba, akili za kujitafutia zinatoka wapi?
 
Back
Top Bottom