Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wakati mwingine usiogope kuwa peke yako katika baadhi ya mambo,kwani inakufanya uwe na nguvu na kufahamu uwezo wako
Kadri unavyojifahamu wewe binafsi ndio utagundua hauhitaji mchango wa watu wengine
Tunapata hofu pale tunapokaa tu lakini tunaishinda hofu kwa vitendo
Simama na pambana na hofu yako kabla haijakushinda
Ukitaka kufanya makosa basi omba ushauri kwa kila mtu
Kuwa makini pale unapojiongelesha mwenyewe kwani huwa unasikiliza pia
Utapata majaribu katika maisha kabla maisha hayaja kubariki
Miujiza ambayo huwa unaitafuta ipo katika kazi au mambo unayo yakataa
Ukijiona kama unajiuliza mara kwa mara kama jambo fulani ni sahihi,basi jua jibu ni hapana
Kutojiwekea mipaka katika maisha ni kukaribisha kutokuheshimiwa
Ni hayo tu!