90% ya wafanyakazi wa Serikali wanapiga soga na story maofisini. Je, tunawalipa mishahara ya bure?

Ofisi zingine zimejaa Watumishi wasio na kazi za kufanya. Na Bado wanasema Wana Shortage ya Watumishi. Job description hakuna. Wengine wanafanya kazi ambazo siyo zao na vitengo wameundiwa. Utumishi Hq hawana muda wa kukagua Watumishi wanachofanya zaidi ya kuwaambia wajaze Opras zisizokuwa na Faida. Ofisi zingine Maafisa Utumishi ndio Mungu Watu Kwa Sababu wamapewa Ruksa ya kuangalia taarifa na Siri za Watumishi. Wana Nyodo wanaokaa Ofisi Moja miaka nenda Rudi bila transfer. Hivyo kujiona wao ndio top Kwa kuwabania wengine hatima zao. Utumishi wake Up please.
 
Sasa kama hawalipwi vizuri watakuwaje na morali ya KAZI.kwa akili kama hizi viongozi wabovu wataendelea kutuongoza.
 
Hao jamaa huwa wanaboa sana na wanajiona special sana, umeandika facts, pia sioni kazi ya wakuu wa mikoa na wilaya maana wapo kisiasa tu kama una RAS na DAS, tupunguze matumizi mabaya ya Serikali
Ni mfumo ovo sn wa CCM
 
Unamaanisha kua kila inapofika ijumaa ofisi za serikali hufungwa mapema hadi j3? Mfano kituo cha polisi,hospitali,shule,walinda mipaka ya nchi(JWTZ) nao hurudi mapema lindoni,Tanesco nk
 
Alafu hii kasumba ya kumpa mtu ajira eti atastaafu baada ya kufika miaka 60 ina tija gani kwa Taifa?
Watumishi wafanye kazi kwa mkataba wa miaka 5, akifanya vizuri anaongezwa mkataba.Wanaopaswa kupewa muda mrefu ni madaktari na Walimu pamoja na Askari.The rest mwendo wa special task contracts tu.
 
Hawa wanatakiwa wapewe mikataba ya miaka 5,kuwepo kwako serikalini kutategemea performance yako,siyo kulea watu wavivu waliopewa uhakika wa ajira mpaka miaka 60!!!
Walimu, Madaktari na Askari ndiyo wapewe mikataba ya motisha mpaka 60 years basi.Vinginevyo tutaendelea kuajiri wakina Mwajuma Ndalandefu na Abunuasi!!
 
Japo na wao pia wanakatwa kodi kwenye mishahara yao Mkuu sio hao uliowataja tu
 
Hao wafanyakazi pia mjue Wana akili, wanasoma huo wivu wenu jju Yao. Kazi kubwa huendana na maslahi Bora. Unataka walipwe kidogo, au uchumi ukue ndo waongezewe mishahara, halafu wakati huo unataka kuwaona walifanya kazi muda wote? Acha wafanye kazi kwa kadri wanavyolipwa. Uchumi ukikua nao watakuza utendaji na uwajibikaji wao.
 
Nilifanya application ya certificate fulan hv mwez wa 11 mwaka jana kwa title ya mjasiriamali nikakamilisha kila kitu na ada nikalipa certificate nimepata mwez wa 8 mwaka huu
 
Nilende TBS kwa ajili ya certification ya product pale HQ niliwakuta wanapiga story huku wanajishika vitambi mm mjasiliamali nifanyaje nikawa kila ninayempa tatzo langu ananitajia room ya kwenda kuulizia aice nilichoka siku hyo
 

Hii survey imetumia sample yenye ukubwa gani kuwakilisha watumishi wote?
 
Maskini mna shida sana, badala u uhangaike na wanasiasa wanaopata mara elfu ya hao watumishi unataka kuangamiza maskini wenzio. Stupid.
 
Wewe unagongwa. Malipo kidogo unataka wafanyeje
 
Wakirudi utawasikia I was veri veri bize today

Ova
 
Mabadiliko ni jambo lisilozuilika. Utachelewa ila litafika wakati wa kutakiwa kutokea litatokea tu.

Haya malalamiko yenu ni matokeo ya serikali kutokuweka maandalizi mazuri ya mapokeo ya kwaajiri kizazi chetu walirelax tu wakijua maisha yatakuwa hivi hivi miaka yote hakutakuwa na mahitaji makubwa ya ajira.

Wakati umefika watoto wameshakuwa watu wazima wanataka sasa kushika nafasi zao katika taasisi muhimu za kitaifa ili washiriki katika kulijenga na kukiendeleza taifa lao. Zinaanza porojo sasa, mara oooh vijana taifa la kesho, mara oooh vijana mjiajiri, mara ooh, mikopo kwaajiri ya wajasiriamali, mara oooh sensa ... Hizi kelele zote ni kukwepa swali la msingi.

Swali la msingi linahoji KWANINI HAPO SERIKALINI SURA NI ZILE ZILE KWENYE UONGOZI NA HAKUNA UTENDAJI BORA?

KWANINI HAPO SERIKALINI KUNA WATU UMRI WAO NI ABOVE MIAKA 55 WANAZUNGUKA ZUNGUKA HUMO OFISINI WANAUWEZO GANI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA KISASA ZA INCHI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kweli una uchungu, ungeongelea wabunge wanaosinzia na kugonga meza tu, hao ni wanyonyaji namba moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…