A Boiling Conflict Between Rwanda, Uganda, and Burundi.



This makes me think.
Kikwete was a strong and stable force behind, when it came to handling the politics of the Great Lakes Region.
At least we could sleep peacefully and have assurance of the following day, in those 10 yrs he was in power.
Sasa, with the current adm. and on top of all this going on...Asalaaleeh!

(I stand to be corrected)
 
i concur!
 
Mr slim hajaaminiwa na Watz hata Jpm hajamwamini.
Jenga ratiba zake za kututembelea hapa kwetu utaona ni baada ya vifo vya walinda amani kule Kongo na wakati tukijiandaa kufanya tunachokijua ndio uliona akaja fasta hapa kwetu,na akaahidi kujenga reli kule shinyanga na alipotoka akaja mjumbe wake kuleta mikataba kadhaa na ndio maana uliona mambo yaliisha ila ile ndio ilikuwa kiama yake.

So hakuna anaemwamini hata mmoja hivyo yaacheni tu kama yalivyo
 
tia nyama hapo kwenye kujiandaa kufanya tinachojua...
 
JPM amerudisha mahusiano na Rwanda kwa faida za kiuchumi tu lakini anajua kila nukta ya uhalisia. Pamoja PK na YM kuwa na uzoefu wa regional politics lakini wanajua JPM kazungukwa na manguli/walimu wao akiwemo Mzee Mahiga.
 
DGSE, FRENCH External Intelligence Agency.
How come wanaonekana kujishughulisha na Internal Affairs za baadhi ya nchi za Great Lakes Region?!, halafu sio kujisghulisha tu, mpaka ku spill the beans, i.e the allegedly assassination plot ya Museveni?
Hapa kwenye ukanda wetu kuna mataifa makubwa kama manne hivi pamoja na makampuni makubwa yao yanayoleta pua zao.
 
Kikwete, who had earlier served as the country’s Intelligence Chief and Foreign Affairs Minister

JK hajawahi kuwa Mkuu wa Usalama

Kuwa Intelligence Chief siyo lazima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa. Hata jeshini kuna Intelligence Chief, isitoshe kipindi hicho cha miaka ya 70's Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa na wakurugenzi (Intelligence Chiefs) kama wanne hivi chini ya Mkurugenzi Mkuu......
 
Ni kweli JWTZ is the best army we should be proud about
Is the" best" kwa kutumia vigezo gani? Au unatumia uzalendo wa ki ujaama wa kusifia cha kwako hata kama ni kibovu.
 
Is the" best" kwa kutumia vigezo gani? Au unatumia uzalendo wa ki ujaama wa kusifia cha kwako hata kama ni kibovu.
Kama huijui tasisisi ya JWTZ basi ni afadhali unyamaze usilete siasa za kupingapinga kila kitu. JWTZ ni jeshi imara liliojengwa na kusukika haswa. Inawezekana unakutana na wapiganaji wachache mitaani ukawaona goigoi, lakini jeshi imara hutokana zaidi na uongozi wake siyo idadi ya wapiganaji wala ukali wa silaha zao. Nikikurudisha nyuma sana miaka hiyo ya sabini, Uganda ilikuwa na silaha nyingi sana tena za kisasa sana ilizopata siyo kwa kuuza shaba yote kwa Urusi na kupewa silaha hizo bali hata kwa kuletewa silaha za kisasa zaidi kutoka Libya. Vile vile jeshi lilikuwa kubwa sana kwa vile amini alikuwa akiwekeza katika jeshi tyu, na zaidi ya yote akaletewa wapiganaji zaidi kutoka Libya. Lakini jeshi hilo halikuwa na uongozi uliosukika, na utakuwa umeshakia yaliyowapata. Vita hupangwa na makamanda, wapiganaji hufuata mipango hiyo; na kwa upande huo makamanda TWTZ ni moto wa kuotea mbali sana;usisogelee kwenye anga zao.
 
Huja jibu swali unatumia vingezo gani kusema JWTZ ni bora Africa mashariki na Kati, kigezo cha miaka ya 70 sio kigezo....uwezo wa jeshi lolote unaendana sambamba na uchumi wa hiyo nchi ndomaana unaona Marikani, China Israel uingereza nk wana uongoza kwakua na jeshi bora duniani......sasa Tanzania inayo zidiwa kiuchumi na Kenya karibu mara mbili itakuaje na jeshi bora kuliko Kenya au Congo.....huo ni muujiza gani?
 
israel ana uchumi imara!!?
 
Mmmh!!!! Sijui uwezo wako wakuelewa mambo ya nshi za nje kama bado unahoji uchumi wa Israel
labda ungetafiti wewe uwezo wako ws kuelewa mambo ya nje..maana ulitaja chumi mbili kubwa duniani ukaipachika na israel humohumo..wakati top five haimo..lakini zilizomo top 7 ukaziacha
 
Mmmh!!!! Sijui uwezo wako wakuelewa mambo ya nshi za nje kama bado unahoji uchumi wa Israel
Fuatilia tena vizuri, Israel inapewa msaada wa zaidi ya Billioni 2 USD kwa mwaka kwa ajili ya matumizi ya kijeshi tokea mwaka 2009. Kibaya zaidi juzi Marekani wamekubali kutoa tena msaada wa Billion 38 USD kwa Israel kwa kipindi cha miaka kumi ijayo, ambapo kwa mwaka Israel atakuwa anatumia zaidi ya Billion 3 USD kwenye silaha peke yake.

Hivi unadhani Israel ana uchumi gani wa kutumia Billion 2 USD kwa mwaka ??? Hebu tuache ubishi usiyo na mantiki.

Nakubaliana kabisa na wewe kwamba uchumi una sehemu kubwa sana katika kujenga nguvu ya kijeshi. Lakini uchumi peke yake haujengi jeshi Imara mzee, kuna sababu nyingi tu zaidi ya Uchumi zinazofanya jeshi liwe Imara.

Tena kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko makubwa sana kwenye uwanja wa vita (Evolution of means and methods of warfare) huwezi kusema kwamba uchumi peke yake ndiyo kila kitu. Siku hizi mwanajeshi anaweza kuwa na kompyuta yake sehemu na anaweza akasababisha madhara makubwa kwenye mifumo ya kiusalama ya nchi (Cyber Warfare).

Au makundi ya kigaidi yana Uchumi gani mkubwa kuleta madhara yanayofanyika ulaya ?? Juzi nimeambiwa baada ya kuona teknolojia ya mataifa ya ulaya itawakaba, magaidi wa kiarabu walioingia Ulaya kama wakimbizi wameamua kujigawa kwenye kaya(cells) magaidi watatu watatu ambao hawatumii silaha kubwa bali silaha ndogo ndogo kama visu au mbinu mbaya kama ubakaji na propaganda (Asymmetric Warfare), hivi hili linahitaji uchumi gani kufanya ???


Warfare ni neno pana sana, na utakosea sana kama utaliangalia katika ngazi ya taifa na taifa.
 
Mkuu sawa umeandika vizuri sana ahsante ila unachanganya vitu viwili......kuna kua na jeshi bora ni kitu nitofouti nakushinda vita (battle au war) kua na jeshi bora lazima uwe na uchumi bora, wakati kushinda warfare lazima uwe na mbinu za kijeshi na intelejisia na technology ya jeshi. ambayo pia inahitaji investiment ya pesa.....Isreal ni ya pili kwa uchumi katika mashariki ya kati baada ya saud arabia....lkn inaongoza katika ntelejisia na technology ya vita..... kwahiyo turudi kwetu tunaongoza kipi uchumi au sophiscated military technology au intelejisia ya kijeshi? Jibu ni kwamba baado tuko dhaifu katika kila kitu, labda idadi ya wanajeshi tunao ya kutosha nasalaha za AK47 tunazo tangu zingunduliwe na misrael mwaka 1942.
 
Hivi vijarida vya uongo uongo ni shida sana eti

"Kikwete, who had earlier served as the country’s Intelligence Chief"

Lini JK alikua na cheo hicho kwny nchi hii.
 

Usichanganyikiwe mambo bado.
1.Jeshi bora ndiyo huwa linashinda vita.
2. Ubora wa jeshi haungaliwi kwenye uchumi wa nchi peke yake.
3. Hakuna jeshi linaloshinda vita kwa bahati nasibu lazima mjipange ndiyo mfanikiwe.

NB: Huwezi kutenga mbinu za Kijeshi, Intellijensia na Siasa ya nchi kwenye vita (Holistic Approach)
 
Teh!, eti atarudishwa na nini?
Alivyo mbabe, he'd rather do something else, kuliko kuangukia pua au mikononi mwa adui.

mng'ato yuko wapi apite hapa kuona vurugu nyingine hizi za bestie wake. 🙂
Hahah asante kwa tag mkuu,ngoja niwasome wadau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…