A Call from Egypt πŸ‡ͺπŸ‡¬

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Habari za jumapili,

Basi bana sina hili wala lile, leo sikuwa na mpango wa kuamka mapema kwa sababu kadha wa kadha.

Ghafla nakatishwa usingizi na simu asubuhi asubuhi aaagghhh kuangalia namba mpya. Nikaachana nayo nikarudi kulala nikasema ntaipiga baadae nikiamka.

Baada ya hiari yangu na kupata stafutahi nikashika kilongalonga nirejeshe simu na jumbe zilizoingia. Oohhh laalaah kumbe ile simu ilikuwa ya Ahmes from Egypt.

Huyu Ahmes tulikutana huku Tanzania kwenye tour sites flani hivi. Mie nilienda kivyangu ila tulijikuta tuko kundi moja na tour guide alikuwa mmoja, wao walikuwa wengi.

Sasa macho yake sijui yaliona nini, siku tumemaliza tour akaniomba namba ya simu, sikuona hiana nikampa. Aahahahahaha Ahmes sijui amelewa haluwa, ananialika nikatembelee moja ya maajabu saba ya Dunia Egypt kwa gharama zake.

Na Covido hii hata sithibutu, wali harage bado mtamu πŸ˜…. Nimemwambia afanye maandalizi ntafika huko mwisho wa mwaka (Desemba) nikiwa likizo.




Ila Ahmes anajua kudekeza kwenye simu looh hadi nikajikuta narembua.

Natumai ntachomoka salama...😜

Mahaba Matata.
 
Kasinde

πŸ™‰πŸ™‰πŸ•΅οΈπŸ•΅οΈπŸ˜ŠπŸ˜Š
 
Sasa hivi naitwa Mu-egypt wa Alexandria 😊😊πŸ₯°

Aahahahahhaaaaa ooh laaalaaah...

Wuuuhuuuuuu πŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°πŸ₯°

You know what, I love you more and more everyday πŸ₯°πŸ˜˜πŸ˜˜.

Mu - Egypt mwenye sukari yake aahahahahahaaaaaa.

K’ Matata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…