Aiseee!!!nmejua tofaut tiyar
Tukiendelea ni Kwamba zile ibada za kuchoma pesa kimsingi hazikuwa na mahusiano na Buddhism ya moja kwa moja ndio zilikuwa za siri Mno na hazikufanyika Lila Jumapili bali siku maalum
Kama nilivyosema awali kuwa tuliongozwa na sheria kali kwenye Kila kitu lakini pia tulikuwa na amri tano zinazofanana nyingi na amri kumi kwenye ukristo
1.Usiuwe chochote
2.Usiibe/usimiliki kisicho chako
3.Usiseme uongo kwenye lolote
4.Usizini(labda uandikiwe na Dr Kama tiba)
5.Usitumie kilevi cha aina yoyote
Amri ya kwanza ilihusika na kutokula nyama yaani chochote chenye uhai lakini kuna mazingira ambayo Buddhist aliruhusiwa Kula nyama nayo ni
-Hakuna Jinsi nyingine ya kuishi
-haikuchinjwa kwa akili yako
- hukuona ikichinjwa
-huli kwa ajili ya hamu za mwili
Kwenye amri ya kuiba ilikuwa hivi, Ili tendo la wizi likamilike hupitia hatua kama tano hivi
-Mawazo au fikra za wizi
-kuweka mipango sawa
-kutimiza lengo
-kuficha baada ya kuiba
-kumiliki Kuuza kugawa au kutumia
Amri ya tatu ilikuwa ni kufundishwa kwenda kinyume na mazoea ya kiasili ya ufahamu wa binadamu! Kujitetea kwa kusema uongo na kudanganya. Kwamba ita nyeusi nyeusi au njano njano.....japo kuna mazingira yaliruhusu kudanganya kama kwa njia Hiyo utaokoa uhai
Amri ya nne sisi kama Ma novice hatukutakiwa kabisa kuishi Maisha ya uasherati kwakuwa hicho ni kikwazo kikubwa sana kwenye Maisha ya kibuddha meditation na dhana nzima ya enlightment
Amri ya tano nayo ilikuwa hivyohivyo pombe na vilevi ni kikwazo kikubwa Sana kwenye path ya self cultivation...vilevi vinaharibu akili na kuleta madhara mwilini huku vikichagiza matendo mabaya