Tulimaliza miaka miwili ya kwanza na kurudi Tanzania mwaka ambapo nilikuja kugundua kuwa tayari nimeshadata na mambo ya Buddhism na meditation hivyo kipindi cha kusubiri majibu niliondoka tena kwenda Kenya kupitia Mombasa kwenda kujifunza Krishna consciousness! Hiki ni kitu kipya kabisa. Nilikaa temple ya Mombasa kwa wiki moja tu na baadae kuhamia Nairobi Mathare Rd Hare Krishna temple
Tofauti na kwenye Buddhism tulikokuwa tunachant Buddha's name -Amitofo/Amitoh'una huku tulichant hivi
Hare Krishna hare Krishna
Krishna Krishna hare hare
Hare Rama hare Rama,
Rama Rama hare hare
Hii ilikuwa ni kama salamu na muongozo ambapo kwenye salamu ilikuwa tu ni hare Krishna kama amitofo kwnye Buddhism au Bwana asifiwe kwenye ukristo na salamu alyekum kwenye Uislam nk
Tulikuwa tunachant hare Krishna in deep mpaka mtu unahisi upo dunia nyingine kabisa ni chanting za ajabu sana
Kitu ambacho sikukipenda kabisa kwa wakrishna ni masanamu ya miungu Yao ambayo yalikuwa devilish yakionyesha ukatili mkubwa
Kulikuwa na sanamu la Shetani likichimba kifua cha mtu kwa kucha ndefu kali na kuutoa moyo huku damu zikichuruzika na yule mtu akiugulia mno. Haya mambo yapo kwenye ibada za waabudu Shetani
Sanamu lingine ni lile lenye nyoka na vichwa 12 hili lilikaa/liliwekwa pembe nne za temple na Picha zake kubwa pia
Ukiachana na hayo masanamu jamaa Wana mafundisho mazuri mno na wanatoa Misaada sana kwa jamii ambapo Kulikuwa na kitengo maalum cha kulisha maeneo fukara kilichokuwa kikiitwa FOOD FOR LIFE ambapo tulipika chakula Kila siku na kwenda kugawa mitaani kwa utaratibu maalum. mtaa maarufu ukiwa mtaa wa korongocho huko Kulikuwa na ushetani wote wa dunia hii
Lakini vilevile tulikuwa tunafanya councelling kwa wakora(hawa ni zaidi ya komando yosso).walikuwa wanavuta gundi na petrol ni watu wa kuogofya mno
Kitu cha kushangaza kuhusu Kenya ni Kwamba kuna wakora wengi ni wazungu. Hawa waliharibu kwao na kukimbilia Kenya pale temple tulikuwa nao wanne tuliowatoa mitaani. Kipindi hicho Kenya ilikuwa haifai kwa ujambazi wizi na mauaji ya kutisha. Nakumbuka tulinusurika kifo lakini tukaporwa masufuria ya vyakula tena kwa kutumia matatu
Nilikaa Kenya miezi mitatu nilijifunza Krishna consciousness na kufanya kazi ya kujitolea kwenye kitengo cha food for life Ambako unakutana na maisha ya kutisha kabisa. Watoto wadogo walivyoharibika na kuharibiwa kwa Kila kitu kuanzia kubakwa kulawilitiwa kufundishwa kutumia madawa kuua kuiba nknk.
Majibu yalitoka na tuliofaulu tulirudi South Africa kwa maandalizi ya kwenda nchi za Asia kwa mafunzo ya juu zaidi sasa