chrissleon
Senior Member
- Jul 22, 2015
- 147
- 89
Nipo safarini nikirudi nitafanya hivyo
Nimefanikiwa kukiweka lakini bila picha ambazo bado Ila zitakuja
Nimeiona mkuu kule MMU ila angalia usije ukawafanyia vitimbwi abiria wenzako maana hamuaminiki, mtu akiweza kuishi na wewe lazima awe na uwezo wa kuangalia na kutambua vitu kwa jicho la tatu ndio ata ishi vzr bila ya hvyo anaweza akafikiri anaishi na jini.
Mimi ni mtu mwema sana mpaka natia huruma
Tumalizie simulizi yetu sasa
June ya 1999 tuliondoka Tanzania wanafunzi 5 tuliofaulu kuendelea kwa masomo ya juu zaidi Taiwan, lakini tukipewa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja cha kuzunguka na kufanya practical kwenye temple mbalimbali za Taiwan, Singapore, Malaysia Indonesia, Bangkok Hong Kong nk
Tulizunguka kote huko tukifanya ibada presentations na kujifunza mila na desturi za kibudha kwa kila nchi.....! Tulikuwa na wakati mzuri sana baada ya mateso yote ya South Africa.. Tulifanya mengi kwa kwakweli kuanzia shughuli za kijamii mpaka za kiroho nknk
Kuna tukio la Malaysia hili ningependa nilisimulie pia
Ilikuwa siku moja tunatoka mji mmoja unaitwa Surabaya kurudi Kuala lumpa kwa ndege hali ya hewa ilikuwa mbaya sana na ukikaribia Kuala Lumpur kuna Kilima ambacho husababisha ajali nyingi za ndege.
Ikabidi tuombwe kufanya chanting.. Wanaume tukaingia kazini tukachant ile kikwelikweli.. Nilichant mpaka nikajisahau hatari iliyokuwa mbele yeti. Baada ya kama dk 15 hivi rubani alipata upenyo katikati ya wingu nene na tukatua salama
Mapokezi tuliyoyapata siku ile sitakaa Nisahau..wiki ileile kuna ndege iligonga kile Kilima na kuua abiria wote pamoja na rubani
Tulimaliza kipindi cha mpito na kutakiwa kufanyiwa ordination ambayo ni kuchomwa kichwani dot 3 na moto wa mshumaa mdogo. Vinauma saana na baada ya hapo hizo alama hazifutiki kamwe...kufikia hapo niliomba PO na kurudi Tanzania kuanza maisha mapya uraiani
Ndio mara ya kwanza nimesimulia kwa undani kabisa habari za Buddhism na meditation kuna vingi sijagusia kama habari za Taoism confuscious na sect nyingine ndogo ndogo Zenye mahusiano na Buddhism
Mimi ni mtu mwema sana mpaka natia huruma
Mkuu wakati naishi kisiwani hong kong nlikuwa naona katika baadhi ya mitaa ya makazi ya watu kunakuwa na visamu vidogo na kubwa pembezoni ya barabara zinakuwa zimewekewa matunda kama machungwa na ma apple. hivi ile ni budhism ama ni imani tafauti?
Kuna kipindi chao mimi sikielewi huwa wanakuja wahindi tofauti tofauti na vyakula, matunda na hata pesa, wanaweka kwa huyo sanamu wao (sielewi nini maana yake).Mkuu wakati naishi kisiwani hong kong nlikuwa naona katika baadhi ya mitaa ya makazi ya watu kunakuwa na visamu vidogo na kubwa pembezoni ya barabara zinakuwa zimewekewa matunda kama machungwa na ma apple. hivi ile ni budhism ama ni imani tafauti?
Yukon hong kong mbali sana chukua hii hapa; pale upanga karibu na makao makuu ya JWT kuna ofisi ya jamaa flani hivi wahindi, hao jamaa wana hilo sanamu.Kuna kipindi chao mimi sikielewi huwa wanakuja wahindi tofauti tofauti na vyakula, matunda na hata pesa, wanaweka kwa huyo sanamu wao (sielewi nini maana yake).
Ila sasa wabongo wanaofanya kazi hiyo ofisi na hata walinzi wakiona jamaa wanakaribia kuja basi hata walio off kiofisi wanakuja kazini! Kwa nini?
Sababu hao wahindi wanapoweka vyakula na mapesa wana_feel huyo 'sijui mungu wao' anakula na pesa kuchukua, basi waswahili usiku wanafungasha kila kitu na kusepa navyo doh!!.
Kazi hiyo mshana jr hupo hapo?
Huko hong kong mbali sana chukua hii hapa; pale upanga karibu na makao makuu ya JWT kuna ofisi ya jamaa flani hivi wahindi, hao jamaa wana hilo sanamu.Kuna kipindi chao mimi sikielewi huwa wanakuja wahindi tofauti tofauti na vyakula, matunda na hata pesa, wanaweka kwa huyo sanamu wao (sielewi nini maana yake).
Ila sasa wabongo wanaofanya kazi hiyo ofisi na hata walinzi wakiona jamaa wanakaribia kuja basi hata walio off kiofisi wanakuja kazini! Kwa nini?
Sababu hao wahindi wanapoweka vyakula na mapesa wana_feel huyo 'sijui mungu wao' anakula na pesa kuchukua, basi waswahili usiku wanafungasha kila kitu na kusepa navyo doh!!.
Kazi hiyo mshana jr hupo hapo?
Hata kule waafrika walikuwa wakikuta zagazaga zimewekwa wanabeba wanaenda kula
titimunda
Doh!! Waafrika bana, yaani hawaachi kitu, au wanaelewa Mungu ni mmoja tu wa mbingunj hizi nyingine ni senema tu.
Sasa comrade hilo dubwana halikuli chakula wala kutumia pesa, so how come uache chakula na pesa ziharibikie pale?Hahahahahaaaaa TODAYS yale madude kama huyaamini halali kabisa kuyasaidia Kula kunywa na hata kuchukua hiyo mihela.kinachokuja kukuumiza baadae ni ile karma ya wizi na sivinginevyo
Hivi mtu mwema anajisema?...ha ha hii kali!Mimi ni mtu mwema sana mpaka natia huruma
Hivi mtu mwema anajisema?...ha ha hii kali!
Hata mimi nmeishia kucheka tu
Umeona eeh!..watu sampuli hii hawatakagi ujinga japo wana masihara mengi.