Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
"A JOURNEY" MY LIFE, SPEECHES & WRITINGS" KUTOKA KALAMU YA JUMA VOLTER MWAPACHU
Kuna wakati naamini hata William Shakespeare alikuwa anaishiwa na maneno kalamu ikabakia inaning'inia mkononi na wino kumkaukia.
Leo nimekitia kitabu mkononi.
Kwa hakika nimechelewa kukipata na sababu ni kuwa nilisubiri uzinduzi.
Kitabu kimetoka na mimi si mtu wa kukosa kuwa na kitabu anachoandika Juma Mwapachu kwani kawaida nakwenda kwenye uzinduzi na nakala yangu inapata saini yake.
Nilijihisi vibaya siku kaka Juma aliponiuliza kwenye simu kama nimekisoma kitabu chake kipya.
Hakika nilijisikia vibaya sana.
Juma Mwapachu ni mwalimu wangu na nimejifunza mengi kutoka kwake.
Nimepagawa.
Sijui nianze vipi.
Nianze kukieleza kitabu kina nini ndani au nianze kumueleza mwandishi?
Msomaji wangu naamini ushajua kuwa Juma Mwapachu ni mtu maalum kwangu.
Juma Mwapachu ni kaka yangu.
Sote tuliokuwa wadogo kwake hivi ndivyo tunavyomwita, ''kaka.''
Kwa wengine wadogo kwake ni kaka lakini kwangu mimi ni kaka na mwalimu wangu na nathubutu kusema ni ''Role Model,'' kwangu kwani tuko nilipofahamiananae mwaka wa 1967 wakati huo ndiyo wanafunzi Chuo Kikuu yeye akiwa mmoja wao wamefukuzwa kwa tatizo la kugomea National Service.
Ulikuwa mwaka wa 1966 na nilijuana na Juma Mwapachu mwaka wa 1967 na.nimekuwa mwanafunzi wake.
Nilikuwa na umri wa miaka 15.
Inatosha.
Nina picha nimepiga mwaka wa 1967 na kaka yangu Juma yumo.
Ilikuwa nyumbani kwa mama yetu, yeye dada kwake, Mary Mackeja, mama yake sasa Chief Edward Anthony Makwaia wa Siha.
Edward Makwaia amerithi kiti cha baba yake Chief David Kidaha Makwaia.
Mimi na Edward tumesoma darasa moja St. Joseph's Convent School.
Edward ambae tumezoea kumwita Ted ndiye aliyenijulisha kwa Juma Mwapachu.
Katika picha hiyo mdogo wake Juma Mwapachu, Wendo Mwapachu yumo.
Siku hii nilipokutana na Juma Mwapachu ilikuwa Birthday Party ya Ted.
Hawa wote niliowataja hapo juu wamo katika katika kitabu hiki kwa maandishi, picha na sura zao.
Kuna picha ni picha na kuna picha na sura za waliomo kwenye picha.
Baadhi ya hawa wametangulia mbele ya haki.
Si jambo la kawaida kuwa kitabu kimeandikwa na msomaji anasoma kitabu na kuyasoma maisha yake.
Msomaji anawajua waliotajwa na anajua waliyofanya.
Sasa nimepagawa kila ninapofungua kurasa.
Situlii kwenye kurasa wala kwenye sura moja.
Mshawasha unanishika nataka kujua sura ya mbele kuna nini?
Kalamu ya Juma Mwapachu inaandika na kusema maneno pia.
Kitabu hiki ni safari kama jina lake linavyoonyesha na mimi nataka nisafiri behewa moja na mwandishi tena nimekaa pembeni yake.
Kitabu hiki kina mengi na kwa hakika ni kamusi tosha ya wanafunzi wa historia ya Tanzania kuwanacho katika maktaba zao kama kitabu muhimu cha rejea.
Nataka niwataje watu mashuhuri wachache ambao Juma Mwapachu kawaeleza kwa kina katika kitabu hiki: Dossa Aziz, Amon Nsekela, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Prof. Ali Al' Amin Mazrui, George Kahama, Dr. Reginald Mengi, Mark Bomani na kaka yake Harith Bakari Mwapachu.
Haya ni mepesi kwangu kuyaeleza lakini yapo mazito ya utawala bora, fedha na uchumi ambayo si mepesi kuyafahamu na kuyaeleza.
Napita kote humo kwa mwenda mkali.
Nimesoma course ya Kiingereza inaitwa, ''Reading Labaratory,'' mwalimu wangu alikuwa mama wa Kiingereza, Mrs. Grant yeye na mumewe Mr. Grant waliletwa Tanzania na British Council kuja kusomesha Kiingereza.
Katika course hii tulikuwa tunafundishwa kusoma kwa haraka bila kupoteza kile unachokisoma.
Hii ni silaha yangu ambayo imenisaidia sana katika maisha yangu ya uandishi.
Napita kuisoma hiyo miamba niliyoitaja hapo juu kwa kasi.
Baadhi ya miamba hii kama Dossa Aziz, Prof. Mazrui, Dr. Reginald, Mengi na Bakari Mwapachu tukijuana.
Kaka yangu Juma ndiye aliyenijulisha kwa Reginald Mengi tukafahamiana vizuri.
Naikumbuka siku hii kama jana.
Dr. Reginald Mengi alimwita mpiga picha wake tukapiga picha.
Sikuwa najua kuwa Mengi na Juma Mwapachu walikuwa marafiki wakubwa.
Juma Mwapachu alinipeleka kwake ili nifanye tafsiri ya Kiswahili ya kitabu chake alichoandika: "I Can, I Must, I Will."
Mwalimu Nyerere hatukujuana lakini nimeandika historia yake kiasi nimeingia katika orodha ya watu watatu (Dr. Salim Ahmed Salim na Brig. General Hashim Mbita) mimi nikiwa wa tatu wao ambao wana taarifa nyingi za Mwalimu katika maktaba zao.
Hili waligundua waandishi wa Nyerere Biography, Prof. Shivji, Prof. Said Yahya Othman na Dr. Ng'waza Kamata wakati wakinihoji kuhusu historia ya Nyerere.
Kitabu kilipochapwa nikakuta hayo na yameandikwa katika kitabu hicho.
Sijipigii zumari.
Dossa Aziz nimemwandika sana pamoja na Mwalimu Nyerere kwani ni vigumu kuandika historia ya Nyerere ukamuacha Dossa Aziz.
Hawa walikuwa marafiki wakubwa kupita kiasi wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Juma Mwapachu alikuwa heshi kumtaja Dossa Aziz kila tulipozungumza historia ya uhuru wa Tanganyika.
Namsoma kaka yangu Juma Mwapachu na kitabu kinanigeukia mimi mwenyewe na kunisomesha ambayo sikuwa nayajua ya miamba hii ingawa mimi nilidhani sina jipya la kujifunza zaidi kuhusu wazalendo hawa.
Juma Mwapachu siku zote amekuwa mwalimu kwangu na kwa jamii ya wasomi wa Tanzania.
Ndani ya kitabu hiki kuna orodha ya vitabu na makala za kisomi alizoandika katika maisha yake.
Utachoka.
Kama nilivyotangulia kusema kitabu hiki ni kamusi ya historia ya Tanzania katika mabonde na milima iliyoteremka na kupanda.
Kitabu hiki ni kamusi ya kuwasoma baadhi ya watu mashuhuri Afrika ya Mashariki ambao Juma Mwapachu aliingiliananao akiwa mtumishi wa serikali na pia akiwa katika sekta ya biashara huria na wakati akiwa Balozi, na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Hiki ni kitabu kizito cha aina yake.
Kuna mengi msomaji atajifunza.
Kitabu hiki kimesheheni mambo mengi ambayo hawezi kuyapata kwengine kokote.
Juma Mwapachu amefungua mlango kwa wengine wanyanyue kalamu zao kuandika kumbukukumbu zao ili Tanzania iwe taifa ambalo wasomi na viongozi wake wanarejesha katika jamii uzoefu na mafunzo waliyopata wakati wakitumikia taifa hili.