Curtis De Mi Amor
Senior Member
- Jan 9, 2022
- 136
- 514
Angela ni jina lake, alizaliwa mwaka 1984 huko Mara.
Alipata elimu yake kwa shida sana ingawa alipambana kwa jasho, damu na machozi. Amepitia changamoto nyingi za kumvunja na kumkatisha moyo, ikiwemo kukeketwa na mimba za utotoni.
Angela alipata mimba alipokuwa shule lakini hakukata tamaa aliendelea kupambana ingawa alikumbana na vipangamizi sana ila alikuwa ni mwanamke wa shoka. Alifanikiwa kufika chuo ambapo aliumwa sana na alipopima aligundulika tayari ana maambukizi ya VVU. Hilo halikumkatisha tamaa na alipambana mpaka akamaliza chuo.
Alienda mtaani ambapo alianza kujishughulisha na uuzaji wa mitumba ijapokuwa biashara haikuwa nzuri hivo alipata hasara na kufilisika. Baadae alianza na biashara ya nguruwe kuwatoa vijijini na kuwaleta mjini. That was her breakthrough! Ilimfaidisha sana kisha akaingia kwenye kununua mbaazi, maharage na karanga na kuzileta mjini.
Kwakuwa alikuwa na malengo yake aliamua kufungua NGO yake kwa lengo la kupinga ukeketaji, ndoa za utotoni, mimba za utotoni na mapambano dhidi ya UKIMWI. kila siku Angela hutembea kilomita zaidi ya 20 kwaajili ya kutoa elimu kwenye jamii huko Mara.
Naam mwitikio umekuwa mkubwa sana kwenye jamii na sasa wengi wameanza kuacha hizo mila na dhana potofu! Angela hajaolewa mpaka leo ila ana mtoto mmoja ambaye anamsomesha mwenyewe, amejenga nyumba 2 ana usafiri wa kutembelea na hivi karibuni ameizindua ofisi mpya ya NGO yake. Ni mwanamke wa mfano mwenye ujasiri na moyo wa kujituma.
NB: Wanawake wanaweza hata wasipowezeshwa wapo wengi ambao wanahisi kukwama ila Angela anawaambia safari bado endeleeni msife moyo!