Kuna thread jana niliwaambiwa mnapotaka kujua mambo ya kanisa katoliki basi inabidi mjipinde kusoma. Kwa mvivu wa kusoma na bingwa wa kuropoka basi kwa Kanisa katoliki utakuwa unaumbuka kila siku.
Wenzenu magazeti ya Ulaya na America wameweka waandishi maalumu kwa ajili ya kusoma na kulielewa kanisa katoliki na inapotokes issue ya Kikatoliki hawawi wababaishaji.
Inaelekea ndoa hii itafungwa kanisani. Kama ni hivyo basi kanisa Katoliki huwa linaangalia mambo yafuatayo.
Kwanza ndoa ni Sakramenti ambayo padre haitoi bali mke anampa mume na mume anampa mke. Ukishapewa Sakremant basi haiondoki hadi kifo chako.
Kitakachofanyika ni ndoa kutangazwa kama kuna kipingamizi. Na vipingamizi ni hivi kwamba labda mhalifu alifungia ndoa jimbo lolote duniani halafu akaja jimbo jingine na kudanganya.
Kinachotakiwa hapo ni kutaja tu diocese mtu aliyofungia ndoa na wala huna haja ya kuleta ushahidi kwani padri wa parokia {Paroko} iliyofungwa ndoa atapigiwa simu na kujulishwa alete kopi ya rekord za ndoa ile.
Kama hakuna kipingamizi hakuna kizuizi cha kuzuia ndoa isifungwe.
Kwa Dr. Slaa na Josephine sijajua watafungia ndoa yao jimbo gani. Lakini kwa sheria za kanisa Dr. Slaa hajafikisha miaka mitano ya makazi yake jijini D'Slaam, hivyo nasita kusema kuwa kikanisa yeye ni mkazi wa Archdiocese of D'Salaam.
Ni wazi bado anahesabika kuwa yeye ni Maktoliki wa Jimbo la Mbulu kwa Askofu Beatus Kinyaiya na si mkazi wa D'Salaam kwa Askofu Polycarp Pengo.
Hivyo hata kama ingekuwa issue inapelekwa kwa askofu ni ujinga kuipeleka kwa Pengo wakati Dr. Slaa hajawa muumini wake. Ningemuona huyu jamaa ana uelewa kidogo kama ningesikia anadhamiria kumuona Askofu Kinyaiya.
Lakini je anatakiwa kufikisha kwa askofu?
Ukweli ni kwamba wanaomuelekeza huyu mtu wanazidi kumpa Dr. Slaa sifa. Wanasahau kwamba Dr. Slaa ni mtaalamu mkuu wa Sheria za kanisa Katoliki katika level ya Phd. Ikibidi Dr. Slaa anaijua vizuri Sheria za Kanisa kuliko maaskofu wengi ikibidi kuliko wote.
Hivyo, nikisikia kuwa anafunga ndoa Kanisani sishangai na najua haitakuwa na kipingamizi.
Vilevile suala hili ni dogo sana ambalo liko mikononi mwa Padri atakayewafungisha ndoa. Usipolielewa kanisa Katoliki unaweza kudhani kwamba Askofu ni kama bosi wa Jimbo hivyo anaweza kuzuia sakrament.
Sivyo. Sakrament hutolewa na padri kwa niaba ya Yesu hivyo hakuna mtu hapa duniani wa kuzuia kama haina kipingamizi cha imani.
Yeye aende kwa Polycarp Pengo, ikibidi apande ndege hadi Vatican aeleze suala lake. Lakini kama Josephine hajawahi kufunga ndoa ndani y aKanisa Katoliki basi huyu bwana na washabiki wake imekula kwao.
Polycarp Pengo atamkaribisha vizuri, atapewa juice, chai na keki kama zipo. Ataona sanamu nyingi nz nzuri za Bikira maria zilivyopambwa pale na Rozari, kisha Pengo atakuja.
Wataongea naye na Pengoa atakachofanya atamfundisha katekism ya Kanisa katoliki kuhusu mambo ya ndoa. Ikibidi atamshauri aonyeshe upendo kwa kuhudhuria misa ya ndoa ya Mkatoliki aitwaye Wilbrod Slaa na Josephine Mushubusi.