A stingy man Will make a stingy husband (Wanaume ubahili sio sifa nzuri)

Kama ilivyo kwa mkate mgumu mbele ya chai

Duniani Hakuna mwanaume bahili KWA mwanamke anaempenda.

Ukiona mwanaume Ni bahili kwako, ujue hajakupenda.
Ila wengi husema hapa hawawezi mpa mwnaamke yeyote pesa.
Na kama mtu hujampenda upo nae wanini ?
 
Ningekuwa na Girlfriend ningelijibu hili swali lako
Ndio maana unahonga.Ukiwa na girlfriend ni mnapeana. Ukisema una muhonga na yeye siku akikupa/akikusaidia maana yake nae amekuhonga which is not true.
 

Dah aliwekeza ukampiga chin.
 
Asante hii tushalijua mtu bahili kama nini afu niendelee kujitesa? Siku hizi am playing safe. Sitoteswa na haya uloandika hapa.nikiona hivyo nakuchora tu huku nikiangalia plan B.
 
Ndioo muache jamani sio vizuri.
Wewe dada uzi wako umenikumbusha mbali sana kila ulichoandika nime note point. Kati ya point zote hii ndo nimeinote haswaaa

" hana future na wewe kwa nini awekeze kwako?"
From now ka hela kangu katabaki kuwa kangu hayo ya kujipendekeza ati sijui zawadi hapana,

Mtu bahili afe na ubahili wake.
 
Tatizo kabla ya kumuita mtu bahili wewe ulitoa nini....?

Nikufungue tu akili hata wanaume tunapenda zawadi asikuambie mtu . Ulishindwa hata kumnunulia vest au soksi.....? Na ukaona yeye atakununulia nini.....?

Nilicho kiona kwako ni hiki wewe kwa huyo mwanaume ulijiweka matawi ya juu na ndio alivyo kuchukulia Ila ungekua muwazi na real life yako wanaume tunahuruma sana angekupa unavyo taka.

Kama hivyo vyote hapo juu sio basi ulikua treated kama kipozeo flani hivi au malaya flani hivi ndio maana alikua hana story nyingine na wewe zaidi ya sex
 
Kwangu mimi ubahili una connections na kipato cha mtu. Nakumbuka kipindi niko mdogo nilikuwa sipewi hela ya shule.

Life was so hard kiasi cha kwamba hela ilikuwa napata nikitembelewa na shangazi au na wajomba ndio wananitoaga. Basi ile hela naitumia kwa mahesabu kichizi kiasi kwamba nilikuwa siwezi kutoa hela kwa kitu ambacho hakinifaidishi binafsi.

Nadunduliza chenji chenji nanunua vitu vidogo navyopenda ila watoto wenzangu kwao kutumia elfu 5-10 kwa siku ni kawaida wengine wanakuja na magari shule wengi watoto wa kihindi na kiaarabu.

Ila by the time nafika chuo nikawa na access na malaki. Then i knew it kuwa kumbe mie sio bahili ila ni umaskini tu ndio ulikuwa unanisumbua. Nilichojifunza ukiwa una mkondo wa uhakika wa kupata hela huwezi kuwa mchungu kutumia au kushea na unaowapenda. Ukiona una mahela mengi na still una uchungu wa kuzitumia jua wewe una roho ya kimaskini na choyo.
 
Kweli kabisa wengi wanashindwa kuoa..mikono yao mizito kutoa, anawaza kuhudumia familia anaogopa.
The issue sio kutoa? Je, unacho hicho cha kutoa? Tunawaingiza wengi kwenye dhambi ya ubahili ila kimsingi ni kwamba hamna mwanaume ambaye hatoi hela kwa mpenzi wake ikiwa anazo. Ukiona hupewi jua uchumi wa mtu ni mgumu aidha hana kazi ama anaunga unga maisha.

Exceptions ni za wachache sana amabao hata sisi wanaume wenzao tunawashangaa. Mtu ana hela ila hata kujipenda kuvaa smart tu hawezi. Ila ana mshahara wa 2M kila mwezi.
 
Nashukuru sana kwa Dua zako X wangu, inshaallah mungu amesaidia hapa nilipo sina jinsi zaidi ya kushukuru. Japo nilipenda tungekuwa wote ila sasa nimejaaliwa mke na watoto wazuri. Maisha ni safari lakini yote mipango ya mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…