a = TANZANIA: SABABU ZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 KUWA MABAYA NI HIZI HAPA: &&&&&&

Makomangilo

Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
20
Reaction score
3
  1. Shule za sekondari kuhamishiwa TAMISEMI. Watendaji wa Tamisemi badala ya kusimamia taaluma mashuleni, wanasumbua na kuharibu taaluma kwa (a) kuingilia utawala wa shule katika kuendesha shule; (b) kusumbua na kusambalatisha walimu kila wakati ambapo wanawakatisha tamaa na kuwaondolea utashi 'Morale' wa kufundisha (c) kukata au kuwanyima mafao yao kwa makusudi.
  2. Wanafunzi kutotimiza majukumu yao ya kujifunza. Jamii na wazazi waelewa kuwaacha tu watoto wao kuendelea na uzembe.
  3. Wanafunzi kutokuwa na nidhamu mashuleni na jamii kuwakingia kifua wanapokosa wasipewe adhabu. Kitu hiki huhamisha fikra za mwanafunzi kuwa mtii katika kusoma na kuwa kichaa na mwenye kibuli.
  4. Watoto kuachiwa kutumia simu mashuleni na maeneo mengine ambapo muda mwingi husikiliza muziki, au huchati na rafiki zake au hupiga simu za kutongozana na wapenzi wao. Muda huu ambao ni wa manufaa kielimu hutumika isivyo. kwa mwanafunzi kuacha kusoma na kufikiria kusoma hawezi kufaulu mtihani. Mwanafunzi ameweza kuandika wimbo wa muziki kwenye mtihani ambayo ni kazi ngumu ya kutumia akiri nyingi; kumbe akiri hiyo hiyo ageihamishia kwenye somo la kiswahili angeweza kufaulu hata kama hakuna mwalimu. wimbo wa muziki ameandika bila kufundishwa, hata kiswahili angeweza kujifunza bila mwalimu kwa kutumia vitabu na muhitasari.
  5. Walimu kutolipwa mishahara inayoshotosha mahitaji yao kama wafanyakazi wengine wenye elimu sawa na wao, mfano TRA, AFYA N.K. Hii ingewafanya walimu watulie, wafanye kazi ya ualimu vizuri na kuwaza namna ya kuwaelimisha wanafunzi kwa matokeo ya kufaulu.
  6. Walimu kutotambuliwa na kuheshimiwa na jamii. Jamii inawanyanyasa sana walimu kwa sababu ya msalahi yao duni. Inafikia mahala baadhi ya walimu akiulizwa na mtu ambaye hamufahamu kuwa anafanya kazi gani, huficha kazi zao na kutaja kazi zingine zenye masilahi makubwa ili kulinda heshima ya utu wake au ili apatiwe huduma nzuri. Kitendo cha mwalimu kutotambuliwa na jamii naye anaondoa wito wake wa kufundisha wanafunzi. Anabakiza tu kuingia darasani kama muhubiri ambapo wasikizaji wake hana shinda ya kuwapima kama wamemwelewa na yale aliyosema wameyashika au la. Dawa ni kuwalipa walimu malipo yanayowatosha kuishi vizuri. Mtu fukara katika jamii hana thamani kwa watu kiushirika (social life).
  7. Ukosefu wa walimu wa hisabati, sayansi, maabara na vifaa vya kutosha vya maabara katika shule nyingi za serikali. Watoto wawapo shuleni, wanatakiwa wajifunze mafunzo yaliyopangwa kujifunza wakati ule ule uliopangwa kujifunza. kwa sasa watoto hawajifunzi wakati ule ule ulipangwa na wengi hawajifunzi kabisa. Mwanafunzi anapofanya mtihani wa somo ambalo hakufundishwa ipasavyo au hakufundiwa kabisa, hawazi kufaulu bali hufeli.
  8. Hakuna mtaala wa elimu wa kudumu unaoeleweka Tanzania (clear and consistent curricurum for all Tanzanian schools). Kwa kuwa mtaala haueleweki, syllabuses nazo hazieleweki. kwa kuwa syllabuses hazieleweki, vitabu na vitu vingine vya kufundishia masomo navyo havieleweki. Mfano: Kwenye somo la Geography, Mtihani wa mwaka 2012 (csee - SCHOOL CANDIDATES); swali la 6 ambalo ni la lazima; Mtunga swali ametumia syllabus ya 1997 hali syllabus iyotumika kufundishia wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 katika shule nyingi za Tanzania ni ya 2010. Swali linahusu LEVELLING IN LAND SURVEY. Topic hii haipo kwenye syllabus ya 2010 bali ipo kwenye syllabus ya 1997. Kwa hali hiyo basi, wanafunzi walioweza kufanya swali hilo, ni wale tu waliofundishwa na mwalimu aliyelitunga na wale tu waliofundishiwa syllabus ya 1997. Wale wa shule za KATA na za kawaida hawakuweza kulifanya, kwa hiyo wakafeli. Yapo mapungufu mengi sana ukiyachimbua. CHA KUANDIKA TU NI KWAMBA, MSIMAMO IMARA ULIOTULIA WA ELIMU TANZANIA HAUPO, NA KWA MAANA HIYO WANAFUNZI WALIOWENGI HAWAWEZI KUFAULU HATA KAMA WAKIWA NA UWEZO MKUBWA KIAKIRI. MPAKA USANII NA UBABAISHAJI UONDOLEWE NDIPO ELIMU TANZANIA ITAKUWA BORA.
  9. Tatizo lingine ni utofauti wa walimu wanaofundisha masomo. Mwalimu wa somo fulani aliyetoka UDSM ni tofauti na aliyetoka UDOM, ni tofauti na aliyetoka MWENGE, ni tofauti na aliyetoka SEKUCO, ni tofauti na aliyetoka SOKOINE, ni tofauti na aliyetoka RUCO, ni tofauti na aliyetoka ............... Hii ni kwa sababu hakuna usawazishaji wa mitaala na course contents inayofundishiwa katika vyuo vikuu vya elimu Tanzania. Matokeo yake ni kwamba watoto wanakuwa wanaeleweshwa tofauti tofauti. Kwa maana hiyo, kwenye mtihani wa Taifa, wanafunzi watakaofaulu vizuri ni wale tu watakaofundishwa na walimu waliotoka katika chuo kikuu alichosomea mwalimu mtunga swali. TANZANIA HAKUNA MTAALA NA UTARATIBU WA ELIMU UNAOELEWEKA. Hii nayo ni mojawapo ya sababu zilizochamgia wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 kufeli.
 
Mleta uzi pokea my like. Ila badili, wingi wa syllabus ni syllabi na si syllabuses. Kweli silabas za vyuo vikuu kuna haja ya kuiunganisha ili wahitimu wote angalau wafanane japo si rahsi kwa sababu za kibinadamu. Pia, matumizi ya simu mashulen wadau wote wa elimu wanatakiwa waungane ili kulidhibiti na si kuwaachia walimu pekee. Suala la mazingira ya kujifunzia yaboreshwe, matokeo ya mwaka jana tumeyaona lakin hadi sasa sijaona juhudi yoyote ya kuweza kuzuia yasijirudie tena zaidi ya kupeana ulaji wa bure katika tume kwa mambo yanayofahamika. Wazazi tuiamshe serikali yetu kwa kupaza sauti kwamba, sasa baaaasi maana watoto wa wakubwa hawa wako shule zenye viwango vizuri.
 
sababu zote hz Pindaa anazijua ndo maana wenye akili walishangaa anaunda tume ya nn badala ya kufanyia kazi changamoto hzo.au anafikiri atapewa majibu tofauti?tume nyingne ni matumizi mabovu ya kodi zetu.pesa ya tume bora wangetengeneza madawati watt wanaokaa chini tena katikati ya jj nao japo wakalie madawati.UJUHA TU.
 
Nicholaus njoo uone wenzako wanavyotoa hoja zilizo katika mpangilio na zinazovutia kusoma
 
Last edited by a moderator:
Nicholas njoo uone wenzako wanavyotoa hoja zilizo katika mpangilio na zinazovutia kusoma
 
Last edited by a moderator:
Kuna hili jambo la kuwa, ualimu ni sehemu pakee Tanzania watu wanapanda vyeo bila kwenda kusoma. Unatoka grade moja kwenda jingine kwa kuangalia muda tu uliokaa kazini....
 
Mbona hujaongeza na sababu ya Failures kupewa jukumu la kufundisha na kuhakikisha kuwa wanafunzi hawafeli.
 
Mbona sijaona mapungufu ya mfumo wa baraza la mitihan katika ushahishaji na upangaji wa marks kama vile Hoja ya mhe.Joshua Nassary iliyokataliwa kusomwa bungen ambapo inaelezea uozo mkubwa sana,
 
Ndugu Makomangilo umeleta sababu za msingi sana, nami naweza kusema ni karibu 70% ya sababu zote. Hizo 30% nawaachia tume ya waziri mkuu ije na sababu nyingine.

Hata hivyo naunga mkono kwa 100% hizi sababu; 2, 3, 5, 6, 7 na 8. Kusema ukweli nimeziona hizi katika shule ambazo nimefanikiwa kufika au hata kuwa nazo karibu.

Kuhusu hilo la mishahara ya waalimu ni tatizo kubwa, inamaana huyu mwalimu yeye kama mfanyakazi wa afya, KWANINI MISHAHARA YAO INATOFAUTIANA SANA? KAMA ASINGEKUWA MWALIMU, HAWA WOTE WANGETOKA WAPI? Naomba mtu mwenye sababu angalau 5 tu za mwalimu kulipwa mshahara mdogo kulinganisha na mfanyakazi wa afya anitajie.

Vilevile, changamoto nyingine zinazosababisha kuzorota kwa ufaulu ni;

1. Hali ngumu ya kiuchumi.
Hii inasababisha wanafunzi wengine kukosa masomo kwa muda mrefu kwa kukosa pesa za michango mbalimbali ya shule.

2. Mienendo mibovu ya wanafunzi wawapo nyumbani.
Wazazi wa kileo wamesahau kuwa wana wajibu wa kuwasimamia watoto wao wawapo manyumbani, na badala yake watoto wamekuwa wakijiingiza katika starehe mbalimbali na kusahau kujishughulisha na masomo.

3. Pia niongezee katika vitendea kazi (haswa vitabu). Sasa hivi wameibuka waandishi wa vitabu wengi, na vitabu vyenyewe utakuta vingine vina makosa mengi mno na hata vile vilivyosahihi haviendani na mitaala iliyopo. NA HIVI NDIVYO KIMBILIO KWA WANAFUNZI WETU, lakini serikali haichukui hatua zozote.
Kuna mambo mengi lakini kwa sasa niishie hapa.
 
Last edited by a moderator:
hapa suala ni kwa nini matokeo ni mabaya SANA,ubaya wa matokeo upo siku zote ila kwa nini safari hii yamezidi,mambo MENGI yalotajwa hapo juu yapo siku zote,na kufeli kulikua kwa kawaida,ila kwa nini yamekuwa mabaya SANA.

Hapa nitaibua shari,ila ukweli ni kwamba watanzania wengi ni wanafiki na wanaofuata mkumbo kwani kikiibuka hiki wooote tunahama,habari za mwangosi,kuchinja ng'ombe na gesi ya mtwara tumeshayasahau.Hypothesis yangu inaonesha ni mpango uliosukwa maalumu ili kuwasahaulisha watz habari za gesi ya mtwara na bunge kutooneshwa,hapa naexpert kitu kipya na kikubwa kitakacho tuamisha kutoka kwenye mjadala wq matokeo kwenda kwengine.

MUNGU IBARIKI AFRIKA.
 

Mleta uzi have my thumb up...hoja zako ni nzuri lakn watakubana wakuu kwenye credibility of the sourc.
 
Sababu zote hapo juu serikali inaweza kujadili isipokuwa namba 5,maslahi ya walimu. Tusitegemee mwalimu mwenye degree yake analipwa nusu ya mshahara ya mtumishi wa kada nyingine mwenye degree kisha afanye kazi kwa moyo. Hapo tutegemee msemo wa bora liende,
 
Nicholas njoo uone wenzako wanavyotoa hoja zilizo katika mpangilio na zinazovutia kusoma

Haha..inaelekea una allergy na mimi.Kwani wengine kutoa sababau nzuri zinapingana na mimi nini?Kwani ni competition?Huku ni kutoa michango kwa ajili ya kufikia common goal.Unataka niulize kama wametoa solutions pia?
 
Hivi tume ya kuchunguza matokeo imeishia wapi? Pamoja na kupewa dondoo zote hizo bado inashindwa kukamilisha kazi???
 

hivi degree ya medicine inafanana na ya education!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…