"A woman of my dreams" 25years later...

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Wale wakubwa wenzangu mtanielewa vizuri! wakati wetu wasichana warembo walikuwa kwa hesabu. Nilipokuwa shule ya msingi miaka ya '70 nilisoma darasa moja na msichana ambaye kwangu alikuwa a woman of Dream.
Alikuwa msichana mrembo kwa viwango vya wakati ule ambapo maumbile ndio kigezo kikubwa. Aliumbika msichana na tuliomzunguka tulikubaliana kwa hilo. Nilimpenda kweli msichana huyo lakini sikuwa na nafasi ya kuonekana kwake kwa vile alipendwa na hata waliokuwa nje ya shule. Kusema kweli niliungulika sana na mapenzi kwake. Nasisitiza kuwa nilimpenda na nilikuwa na haja naye kiasi kuwa hata ndoto zangu, mipango yangu ya baadae na furaha yangu niliihusisha na yeye. Bahati mbaya sikuweza kumtamkia na nilipomuonyesha dalili alizidharau kwani hali duni was written all over me. Kuanzia kivazi na hata matumizi kwangu ilikuwa tabu. Hata hivyo nilikuwa na sababu moja kubwa ya kuonekana pale shule nayo ni kuwa nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi bora shuleni jambo ambalo lilisaidia kuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya wasichana. Hata hivyo nilikuwa na sifa nyengine nayo ni DOMO ZEGE hivyo sikuwa na uwezo wa kutengeneza uhusiano na msichana yeyote pale shuleni.
Tuliingia Sekondari nikiendelea na ndoto na njozi juu ya huyu msichana lakini hapa hali ya kutonitambua ilizidi kwani tulienda sehemu iliyohitaji hali nzuri zaidi ya maisha. Bahati nzuri nilifanikiwa kuendelea na masomo ya juu na my dream girl hakufanikiwa na wenye uwezo wakatangaza ndowa wakaondoka nae.
Tuliendelea na maisha yetu na Mungu akinijaalia kazi nzuri nami nikafunga ndowa. Ni miaka karibu 25 sasa na kwa nyakati tofauti nikikutana na yule msichana ambae amekuwa mama wa familia. Kwa kuthamini cheo cha ndowa tukikutana humsalimia kwa heshima lakini bado sijasahau niliyvompenda hapo nyuma.
Kipindi cha miezi 6 nyuma nimekutana nae na amenijuulisha kuwa ameachika kwenye ndowa yake na kuanzia hapo ameanza kunionyesha hamu ya kuwa na mimi. Ama kwa upande wangu bado namuona ananivutia na ninashawishika kutibu yale majeraha ya zamani lakini nikiifikiria ndowa yangu nabaki njia panda.
 
Upo njia panda kivipi? Wewe ni mtu mzima na siyo mtoto. Naamini unajua nini maana ya ndowa. Ukiamua kudungua nje ya ndowa ujue linakuhusu . Nawalisema ukionja asali utachonga mzinga. So make wise decision.
 
hahahaa, jipozee machungu ya zamani!
ila sasa itakuwa kibibi bibi na kibabu babu!
 

Hivi fikiria mke wako naye akija na similar story na boyfriend wake na akapanga kudunga nje ya ndoa yake wewe utajisikiaje? Sikiliza brother, wewe sasa hivi una ndoa yako na familia yako, unapaswa kujiheshimu na kuiheshimu ndoa yako na kumheshimu mkeo pia. Dream zako za zamani zisilete kikwazo kwenye amani ya ndoa yako sasa. Yeye anafanya hivyo kwa sababu sasa hivi hana hiyo kitu uliyoiita ndowa lakini kumbuka kuwa wewe upo kwenye ndowa bado hujaachana na mkeo. Angekuwa ni woman of your dream angekukubali inhali ukiwa huna mbele wala nyuma, anakuona unafaa sasa baada ya kuwa na maisha mazuri na kuwa na familia bora na baada ya yeye kupoteza ndowa?!
Hebu tafakari ndugu yangu!
 
Ngoja isubiroe baada ya miaka 2 labda na me my dream girl atakuja kwangu.
maana kaolewa mwaka jana na nahisi huo aliko saa hii atakua na ujauzito ka sio mtoto.
 
Mwaka 1970.........nimeshindwa hata niseme nini...
 
yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo
 
wacha maneno yako wewe",..anavutia! anavutia!..kwan yeye kitegauchumi na ww muwekezaji...heshim ndoa yako..:boxing::boxing::boxing::boxing::boxing::boxing:
 
achana na huyo bibi........
Hiyo siyo 'love' ni'obssesion'
 
Acha kuiweka Rehani ndoa yako

Yeye hana ndoa kwa sasa hivyo kwake lolote ni sawa

Wewe mwenye ndoa ndio wa kuangalia usije kua chanzo cha kuvunja ya kwako, kuwa mwangalifu sana
 
hujajiuliza kwa nini alikudharau that time?? Ujana wake achezee na nani uzee wake amalizie nan? Hahahahahaha. Akili kumkichwa na utu uzima dawaa..
 
Dumping charges or fees hapo umei-consider ? au unataka tu kuparamia ...
 
Miaka 25 ya ndoa, maana yake watoto wako wamo humu na possibly wao ndio wanakupa ushauri; badala ya wewe kuwapa ushauri.

Sidhani kama kuna kitu hukijui, labda unatupa story tu!
 
Hahahahaha, duh una mambo, Em acha kutuenjoy, tunga story nyngne hapa umeprove failure... Acha obsession.za ajabu hzo... We mtu mzima kweli? we ni dogo tu unatutungia ctor.. Post thread za maana bna
 
Tulia kwenye ndoa yako magonjwa mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…