Pre GE2025 A-Z ya kinachoitwa michango ya kumchangia Rais Samia pesa ya kuchukua fomu ya kugombea Urais 2025

Pre GE2025 A-Z ya kinachoitwa michango ya kumchangia Rais Samia pesa ya kuchukua fomu ya kugombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mr RoundAbout

Member
Joined
Oct 6, 2023
Posts
74
Reaction score
89
Wana bodi, ni tumaini langu unaendelea vizuri na sherehe za pasàka pili.

Baada ya kusikia Kwa muda mrefu suala la watu tofauti tofauti kujitokeza na kudai watamchangia Mama pesa za kugombea Urais mwakani, binafsi nilianza kufanya uchunguzi.

Leo asubuhi nimesikia redioni katika Moja ya vipindi vya magazeti kuwa Sasa fedha hizo zimefika kiasi cha takribani milioni 100. Tangu propaganda hii ianze watu binafsi na Taasisi wamejitomeza kufanikisha azma hii TATA.

Maana yake ni Nini?
1. Imebainika kwamba watu wanaofanya hivyo wanajaribu kujenga mazingira ya kuonekana wanamuunga mkono Rais SAMIA Ili na wao waendelee kupata wanachokitaka (give and take philosophy)

2. Kundi hili linaongozwa na makada wa CCM ambao wanataka kuuaminisha umma wa watanzania kuwa chaguo la CCM mwakani ni MAMA wakati ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa.

3. Kundi hili ni wale wanaoitwa CHAWA, ambao wanatumia nafasi hiyo Ili kujinufaisha wao wenyewe Kwa kuutambua udhaifu wa mamlaka

4. Sustainability. Ili uendelee kudumu katika uwepo wa mamlaka hii, basi mtukuze Mfalme hata Kwa UONGO.

5.Hii ni kampeni ya kuwadanganya watanzania mapema kuwa Rais Samia anakubalika, wakati kwenye ground hayupo.

MY TAKE: Najua wahusika niliowataja hapo juu, watapingana na Mimi lakini ukweli ndiyo huo.

Wasalaam..........
 
Ndugu zangu Watanzania, kazi ya URAIS ni ngumu sana

Baada ya Muhula wake kuisha, anaomba tena kura aongezewe Muhula mwingine 🙌
 
Fomu ni moja tu ya urais,na ni ya kwake.
Sasa si tufanyeje🤷‍♂️
 
Back
Top Bottom