Aaaaah TB

Van Mlaki

Member
Joined
Mar 10, 2013
Posts
7
Reaction score
0
Me ni kijana nina mpenzi wangu tuko katika mahusiano miaka minne sasa hapa katkat alisumbuliwa sana na kifua lakin hakuwa anatkwa na makohoz,hospital walikua wanampa dawa za kulainisha hadi juzi(Jpil) kifua kikalainika,jana tukaenda hospital akapiwa TB leo tumefwata majib ni kweli anao...
Mimi nipo ktk hatar kiac gan ya kuambukizwa na ikiwa naishi naye?
Tunaweza kufanya mapenzi au ndo mpaka miezi sita ya matibabu ipite?
Naombeni uxhaur wenu..
 
Mkuu.@Van Mlak Itabidi ufuate ushauri wa Daktari amesemaje huko hospitalini itabidi awe na vyombo vyake vya kulia usije ku share nae vyombo vyake na akiwa anatumia dawa zaTB hawezi kukuambukiza ila uwe muangalifu vyombo vyake vya kulia akimaliza kutumia vioshe kwa maji ya moto uviweke sehemu muhimu. kuhus ku do kamuulize Daktari kam utaweza ku do au hapana lakini wewe hungoji mwenzako apone ndio u do Mapenzi? humuonei huruma mwenzako ana umwa wewe unataka Ku Do?
 
Kifua Kikuu - TB

TB au Kifua Kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na viini viitavyo ‘tubercle bacilli’.
Wengi wetu tuna viini vya TB mapafuni mwetu lakini hii sikumaanisha kwamba tutauguza huu ugonjwa. TB hushika wale ambao wana ukosefu wa kinga mwilini unao sababishwa na kutokula chakula kizuri, matumizi ya madawa ya kulevya au wanaouguza magonjwa mengine.

TB ya mapafu ndio imeenea zaidi. Hata hivyo, viini vya TB vinaweza kusafirishwa kutoka mapafuni kupitia kwa damu hadi sehemu zingine za mwili na kusababisha hivyo viungo viathiriwe na TB.

Viini vya TB hupatikana kwa mate ya muuguzi. Wakati mgonjwa anakohoa, kupiga chafya au kutema mate kiholela, viini vya TB husambazwa kwa hewa. Mwenye afya akiipumuwa hewa hiyo anaambukizwa na mapafu yake inaanza kuwa na vijidonda.

Dalili za TB


  • Kikihozi kisichoisha
  • Uchovu na kuishiwa kwa nguvu mwilini
  • Kupoteza uzito
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Kutokwa na jasho hata wakati kuna baridi
  • Maumivu ndani ya kifua
  • Kuishiwa na pumzi
  • Mate yaliyo na damu au kukohoa damu
Tiba ya TB
Kuna tembe tofauti zinazotumiwa kutibu TB. Dawa hizi hutumika kwa kipindi cha miezi sita au hata zaidi.

Dalili za TB zikingunduliwa mapema, sio lazima mgonjwa alazwe hospitalini.
Hata hivyo,ikiwa ugonjwa umezidi sana, mgonjwa wa TB atakuwa mdhaifu sana na itabidi alazwe hospitalini.

Chini ya Kanuni mpya za utibabu wa TB ulimwenguni, inapendekezwa, wagonjwa wa TB ya kawaida wanapaswa kulazwa hospitalini kwa miezi miwili pekee halafu miezi minne iliyobaki watibiwe wakiwa na jamii zao.

MDRTB ni neno linalotumika wakati viini vya TB vinashinda nguvu dawa moja au mbili zinazotumiwa kutibu TB. Shida kama hii hutokea ikiwa mgonjwa ametumia madawa kwa njia isiotakikana au alianza matibabu akakosa kumalizia ile miezi sita inayohitajika. Kawaida, inachukua miezi sita au zaidi kutibu TB kabisa. Hata hivyo, mgonjwa akianza matibabu, baada ya muda kidogo hujihisi yuko sawa. Ijapo atakatiza matibabu, kuna hatari kwamba viini vilivyo mwilini mwake hujiunda kipya na kujiongezea nguvu hivi kwamba madawa aliyokuwa akitumia hapo mbeleni hayawezi kumtibu tena. TB ya aina ya MDR wakati mwingi haitibiki na mtu ambaye anaugua aina hii ya MDR anaweza kuisambaza vile vile kama TB ya kawaida.

Matibabu ya mgonjwa aliye na MDRTB inagharimu mara ishirini zaidi ya yule aliye na TB ya kawaida. Matibabu ya mgonjwa wa MDRTB yanaweza kuchukua muda wa miezi kumi na nane.

TB ni mojawapo ya magonjwa ambayo huathiri watu walio na virusi vya Ukimwi. Kama una Ukimwi, jihadhari sana usishikwe na TB. Iwapo unajishuku una TB, hakikisha umepimwa na kutibiwa vilivyo.

 
Wote tunaweza kuwa carriers wa vijidudu vya tb,lakini swala la kuugua hutegea uwezo wa kinga yako ya mwili,kama umepata hao wadudu na kinga yako iko juu huwezi kuugua but kama umepata na kinga yako ni mgogoro utaugua.,nakushauri uboreshe kinga yako ili kama umepata au utapata hao wadudu usiugue,pia epuka mazingira yatayokufanya upate kama ulivyoelekezwa hapo juu
 
Hi Van Mlaki,

TB is spread thru the following ways:

• TB is spread through the air from one person to another. The TB germs are passed through the air when someone who is sick with TB disease coughs, laughs, sings, or sneezes WITHOUT covering his/her mouth.
• If you breathe air that has TB germs, you may get TB infection. This means you have only dormant (sleeping) TB germs in your body. These dormant germs are not making you sick, and you cannot pass these germs to anyone else. REMEMBER at some point in our life we have inhaled TB germs and they are in our lungs but not causing disease (dormant TB germs).
• If these dormant TB germs in your body wake up and multiply, you will get sick with TB disease, there are several reasons for these dormant TB germs to wake up and cause a disease.
• TB is a curable disease, the drugs are very effective but if TB is not treated it can cause death if not treated with medicine (anti-TB).

You cannot get TB germs from:


• Sharing drinking containers or eating utensils.
• Saliva shared from kissing.


TB is NOT spread through shaking someone's hand, sharing food, touching bed linens or toilet seats, or sharing toothbrushes.

As soon as the patient start TB treatment then he/she become non infectious and therefore the risk of transmitting to other people is very minimal. For your case, i believe your partner has already started treatment, she is non infectious and please help her to finish continue and finish treatment effectively!

Having sex (making love) is not a contraindication to a TB patient, the important thing is whether she is not very ill!
 
mmh,kijana unapenda ngono.msubiri mwenzio apone na amalize dozi zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…